Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Wazo Michael Mwang'onda amewasha Mwenge wa Mwitongo Nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kutumia Mwenge wa Uhuru katika tukuo ambalo limefanyika Agosti 2 mwaka 2026 katika kijiji Butiama eneo la Mwitongo.
Wakiwa Mwitongo, Mwenge wa Uhuru umepokelewa na familia ya Baba wa Taifa wakiongozwa na Chifu wa kabila la Wazanaki Japhet Wanzagi ambaye ni kiongozi wa familia ya Chifu Burito Nyerere na msimamizi wa familia ya Baba wa Taifa.
Katika tukio hilo pia limeshuhudiwa na mkuu wa Mara kanali Evans Mtambi na viongozi wengine wa Serengeti na vyama vya Siasa.












Comments
Post a Comment