Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
MKUU wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Solomon Itunda, ameungana na majonzi ya Watanzania kwa kuwasilisha salamu za pole na rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba mzito wa kifo cha mume wake mpendwa.
Katika kuonesha utu, heshima, na kuguswa kwa dhati na msiba huo, Mhe. Itunda amefika nyumbani kwa Mhe. Rais visiwani Zanzibar kwa ajili ya kumpa pole na kumfariji uso kwa uso katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mwenza wake wa maisha.
Akiwa msibani hapo, Mhe. Itunda alimpa maneno ya faraja Mhe. Rais na familia yake, akimuombea kwa Mwenyezi Mungu awape subira, afya njema, na nguvu ya kiroho ya kustahimili pigo hili kubwa.
"Tupo pamoja nawe katika kipindi hiki cha majonzi mazito, Mheshimiwa Rais. Tunamuomba Mwenyezi Mungu akutie nguvu wewe na familia nzima, na ailaze roho ya mpendwa wetu mahali pema peponi," yalielezwa sehemu ya maombi na salamu za faraja za Mhe. Itunda.

Comments
Post a Comment