Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma.
Mwenyekiti wa mtaa wa Pwani Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma mkoani Mara Abdallah Edward Kitundu amesema Mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF) ni muhimu kwa Maendeleo na ustawi wa jamii.
Ameyasema hayo Septemba 8,2026 mara baada ya maafisa matekelezo wa hifadhi skimu kutoka NSSF kutoa elimu kwa wakazi wa mitaa ya VETA na Pwani katika kata hiyo.
Abdallah ameeleza kuwa mpango huu wa NSSF una manufaa makubwa kwa jamii kwani ni mojawapo ya njia ya kijiinua kiuchumi na kujiletea maendeleo.
" Uwekaji akiba NSSF ni mzuri na muhimu kwa jamii kwani inasaidia kupunguza utegemezi na ghalama za maisha hapo baadae kwa kuwa mwanachama anapata huduma za matibabu ya bima kupitia michango take anayojiwekea yeye na familia yake".
Ameipongeza NSSF kufika na kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kujiwekea akiba ya baadae na manufaa yake ambayo yanapelekea kupata maendeleo sambamba na unafuu wa ghalama mbalimbali na kupunguza utegemezi usio wa lazima kwa baadae.
Athanas Lukuba afisa matekelezo hifadhi wa skimu amewaeleza wananchi umuhimu wa kujiwekea akiba kwa kuwa ni mojawapo ya kuongeza wigo wa Hifadhi ya Jamii kwa makundi ambayo hayanufaiki na huduma hizi ingawa wanashiriki kikamilifu katika kuchangia uchumi wa Nchi.
" Katika Kusaidia juhudi za Serikali za kupunguza umaskini wa kipato kwa wananchi Serikali awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuwajengea wananchi uelewa mpana na kuhakisha wananchi wanafikiwa na kuwezesha kutambua umuhimu wa uwekaji akiba", amesema Athanas.
Hii itasaidia kuongeza nguvu za uzalishaji mali na kukuza uchumi wa Nchi pia kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kwa Upande wake Philipo Kachinde afisa matekelezo wa hifadhi skimu amefafanua kuwa walengwa wa hifadhi skimu ni
Wananchi waliojiajiri katika maeneo mbalimbali.
Ameainisha walengwa hao kuwa ni pamoja na wanaojihusisha na Kilimo,ufugaji,uvuvi,sanaa mbalimbali,wachimbaji wadogo wa madini,maafisa usafirishaji,
Machinga zikiwemo biashara nyingine ndogo ndogo za
Ususi, uchuuzi masokoni, mama lishe/baba lishe.
Emmaculata Edward Ndege ameipongeza Serikali kwa kuweza kuwafikia na kuwapa elimu hii na kuwashukuru NSSF kwa kutekeleza agizo la mh.Rais na kuweza kufika mtaani hapo na kuwapa elimu.
Amesema elimu hii ina manufaa makubwa katika hatua za maendeleo kwa wajasiriamali kwani uwepo wa huduma muhimu ya matibabu inasaidia kutunza akiba na familia kunufaika kimatibabu.
Amewashauri ambao hawajachukua hatua ya kijiunga hasa Vijana wajiunge kwa manufaa yao ya Sasa na baadae na wafike kupata elimu kwa usahihi na wafanye maamuzi kwa mustakabari wa maendeleo.







Comments
Post a Comment