Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

POLISI WANAMAJI WASISITIZA USHIRIKIANO KUZUIA VIFO VYA KUZAMA MAJI

  Na: Dawati la Habari Polisi Mwanza Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza (MPC) kimeshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kuzuia Kuzama Maji Duniani, ambayo kimkoa yamefanyika katika Ufukwe wa Bismarck Rock, Capri Point jijini humo. ​Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza, SSP Abduhaj Mkombe kwa niaba ya Mkuu wa Chuo, amesema chuo hicho ni mdau mkuu katika kuhakikisha kinapunguza vifo vitokanavyo na ajali za majini katika Ziwa Victoria na maeneo mengine nchini. ​"Sisi kama Polisi tuna dhamana ya kusimamia usalama majini na kuhakikisha raia na mali zao wanakuwa salama. Tumeona ipo haja ya kushiriki kwenye tukio hili ili kuonyesha mchango wetu katika kupunguza vifo vinavyotokana na kuzama maji," amesema Mkombe. ​Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Christopher Ngubiagai, amelipongeza Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama kwa kufanya kazi kwa ushirik...

POLISI WANAMAJI WASISITIZA USHIRIKIANO KUZUIA VIFO VYA KUZAMA MAJI

Na: Dawati la Habari Polisi Mwanza Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza (MPC) kimeshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kuzuia Kuzama Maji Duniani, ambayo kimkoa yamefanyika katika Ufukwe wa Bismarck Rock, Capri Point jijini humo. ​Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mkufunzi Mkuu wa Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza, SSP Abduhaj Mkombe kwa niaba ya Mkuu wa Chuo, amesema chuo hicho ni mdau mkuu katika kuhakikisha kinapunguza vifo vitokanavyo na ajali za majini katika Ziwa Victoria na maeneo mengine nchini. ​"Sisi kama Polisi tuna dhamana ya kusimamia usalama majini na kuhakikisha raia na mali zao wanakuwa salama. Tumeona ipo haja ya kushiriki kwenye tukio hili ili kuonyesha mchango wetu katika kupunguza vifo vinavyotokana na kuzama maji," amesema Mkombe. ​Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Christopher Ngubiagai, amelipongeza Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya usalama kwa kufanya kazi kwa ushirikia...

KATIBU MKUU CCM AONGOZA KIKAO CHA SEKRETARIETI KISIWANDUI, ZANZIBAR

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, akiongoza Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika katika Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui, Zanzibar, leo Jumanne, tarehe 28 Julai 2026.

MALIASILI NA UTALII, NMB WAKUTANA KUJENGA UHUSIANO WA KIMKAKATI

*Na Mwandishi Wetu, Dodoma* MENEJIMENTI  ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utalii Bw. Nkoba Mabula imekutana na kufanya mazungumzo ya kuimarisha uhusiano na uongozi wa Benki ya NMB ukiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali Makao Makuu ya NMB Dodoma Bi. Vicky Bishubo. Mazungumzo hayo ya Kimkakati baina ya pande hizo mbili yamefanyika leo Julai 27, 2026 katika Makao Makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Mtumba jijini Dodoma. Akizungumzia kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Mabula amesema kimekuwa na tija kubwa kwani Benki ya NMB ni wadau muhimu wa Wizara ya Maliasili na Utalii hususani katika kuimarisha maeneo yake makuu ya Utalii na Uhifadhi. “Ugeni huu wa wenzetu kutoka NMB unadhihirisha namna Wizara ya Maliasili na Utalii inavyozingatia umuhimu wa kukutana na wadau mbalimbali kama sehemu ya kujenga uhusiano wa karibu na pia kuimarisha utendaji kazi wa Wizara kwa wadau na wananchi kwa ujumla,” amesema Bw. Mabula. Naye Mkuu wa ...

MAONESHO YA ELIMU NJE YA NCHI KUFANYIKA LEO ARUSHA NA TAREHE 30 MWANZA

 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar GLOBAL Education Link (GEL) imesema jumla ya wanafunzi, wazazi na walezi 1,113 wamefikiwa na kupatiwa huduma kupitia maonesho ya Global Education Fair 2026 yaliyofanyika Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam na leo Jumanne yanafanyika Four Point by Sheraton Arusha na tarehe 30 Rockcity Mall Mwanza. Akizungumza baada ya kukamilika kwa maonesho yaliyofanyika Julai 25, 2026 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa GEL, Abdulmalik Mollel, alisema mwitikio huo unaonesha kuongezeka kwa uhitaji wa taarifa sahihi kuhusu fursa za kusoma nje ya nchi. Alisema kupitia maonesho hayo, washiriki walipata ushauri kuhusu uchaguzi wa kozi, vyuo vikuu, scholarships, gharama za masomo, malazi, visa na maisha ya mwanafunzi katika mataifa mbalimbali. “Mwitikio tulioupata Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam unaonesha kuwa wanafunzi na wazazi wanahitaji mwongozo sahihi kabla ya kufanya maamuzi kuhusu elimu ya juu,” alisema Bwana Mollel. Alisema zaidi ya w...

DKT. MWIGULU AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA AFCON

 WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Mashindano ya AFCON, leo Jumatatu, Julai 27, 2026, ameongoza kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika Hoteli ya Verde, Zanzibar. Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah, ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo. Aidha, kikao hicho kimewakutanisha viongozi kutoka wizara, taasisi mbalimbali za kisekta pamoja na mikoa itakayokuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON yatakayofanyika mwaka 2027.