Na Angela Sebastian; Bukoba Mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba mjini Mhandisi Johnston Mutasingwa ametaja sababu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuomba ridhaa ya kuongoza jimbo hilo ambapo ni kutokana na utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati aliyotekeleza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan. Mutasingwa amesema katika jimbo la Bukoba mjini Dk.Samia ametekeleza miradi mbalimbali katika idara ya elimu,Afya,barabara,maji,standi kuu ya mabasi sambamba na soko kuu la Bukoba ambalo lilikwama kwa muda mrefu kutokana na sababu za kisiasa na kiutendaji. Ameeleza hayo leo katika mkutano wa adhara wakati akiomba kura kwa wananchi wa kata ya Kibeta ambapo uliudhuliwa na mamia ya wananchi,wakeleketwa na wanachama wa CCM wa jimbo jilo. "Kwa heshima na taadhima nawaomba Oktoba 29 mwaka huu tumpe kura nyingi za shukrani Rais wetu ili aendelee kutekeleza miradi hii ya kimkakati aliyoianzisha na kutuletea mingine mipya ambayo itapandisha mara dufu maendeleo yetu" amesema Mutasingwa ...
Marato tv - Sauti ya Jamii