Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanzania Yang’ara Uwekezaji Katika Elimu Kwa Rasilimali za Ndani


📌 Dkt. Biteko asema tafiti zaonesha elimu bora huchangia asilimia 20-30 ya ukuaji wa uchumi

📌 Walimu milioni 17 wa shule za msingi na sekondari wahitajika Afrika ifikapo 2030

📌 Bajeti ya elimu yaongezeka kwa trilioni 1.44 tangu mwaka 2020/21


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopiga hatua katika  matumizi ya rasilimali za ndani na kuwekeza katika sekta ya elimu kwa maendeleo endelevu.

Amesema hayo Septemba 24, 2025 jijini Dar es salaam wakati akifungua Kongamano la Tano la Kimataifa la Elimu Bora lililoongozwa na kauli mbiu inayosema “Kuimarisha mifumo na uwekezaji: Kusonga mbele katika Uhamasishaji wa Rasilimali za Ndani kwa ajili ya Elimu Jumuishi, Bora na Endelevu Barani Afrika”.

Dkt. Biteko ametaja hatua zilizochukuliwa na Serikali kuwa ni pamoja na kutunga na kuboresha Sera, Sheria na miongozo mbalimbali ya elimu, kuongeza kiwango cha bajeti ya elimu kutoka shilingi za trilioni 4.72 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 hadi kufikia shilingi za trilioni 6.16   mwaka wa fedha 2024/2025.

Amesema ongezeko hilo la bajeti limeboresha mazingira na miundombinu mbalimbali ya elimu kwa maendeleo endelevu. Vile vile, Serikali imetanua wigo wa Sera ya Elimu bila malipo kwa elimu ya Sekondari ambapo mwaka 2020 kilitengwa kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 312.08 na mwaka 2024 kilitengwa kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 796.58 ikiwa ni sawa na ongezeko la shilingi bilioni 484.

“Ongezeko hili limeweza kupunguza changamoto za kifedha zinazorudisha nyuma sekta ya elimu na hivyo kuongeza idadi ya wanufaika wa elimu malipo kutoka wanafunzi 14,940,925 wa mwaka 2020 hadi kufikia wanufaika 16,155,282 wa mwaka 2024,” amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza “Pamoja na mafanikio haya, Serikali inaendelea na mikakati mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kutatua changamoto nyingine kadhaa katika sekta ya elimu kwa maendeleo endelevu.”

Amewahimiza wadau wa kongamano hilo kuifanyia kazi kauli mbiu ya mwaka huu ili kufikia utekelezaji wa matakwa ya kimataifa ya kutenga na kuelekeza asilimia 20 ya bajeti ya nchi katika maendeleo ya sekta ya elimu.

Aidha, amesema Afrika ikiwekeza katika elimu bora itaweza kutatua changamoto ya uhaba wa walimu bora hususan maeneo ya vijijini. Ambapo, hadi kufikia mwaka 2030 Bara hilo linahitaji kuwa na walimu milioni 17 ili kuwa na elimu bora ya  msingi na sekondari na kuwa na mifumo thabiti ya elimu ya kidigitali ambayo itasaidia kukabiliana na changamoto zilizopo nakuendana na mazingira tuliyonayo. 

Ambapo tafiti za Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) mwaka 2025 zinaonesha kwamba, elimu bora, kwa wastani, huchangia asilimia 20 hadi asilimia 30 ya ukuaji wa uchumi wa muda mrefu wa Taifa lolote. Tafiti hizo hizo pia zinaonesha kuwa, mtu mwenye elimu ya juu hupata kipato kwa wastani wa asilimia 50 hadi asilimia 100 zaidi ya mtu asiyekuwa na elimu hiyo ya juu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo amesema suala la kugema raslimali fedha na watu vinaweza kuongeza ubora wa elimu na kupunguza changamoto za sekta ya hiyo kwa kushirikiana na wadau.

Naye, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema kuwa Kongamano hilo linalenga kuboresha sekta ya elimu nchini na kuwa Wizara yake ina jukumu la kuhakikisha elimu inayotolewa inakuwa katika viwango vya kimataifa. 

“ Kongamano hili limekuja katika wakati muafaka ambapo Serikali inaendelea kuwekeza raslimali fedha, hivyo mkutano huo utasaidia kugema raslimali fedha ili kuleta mabadiliko katika mfumo wa elimu,” amesema Prof. Nombo.

Meneja wa Kanda wa Global Partnership for Education (GPE), Belay Addise amesema kuwa Taasisi hiyo inajivunia ushirikiano wake mzuri uliopo kati yake na Serikali ya Tanzania tangu mwaka 2013. Ambapo kupitia ushirikiano huo Tanzania imepokea takribani dola za Marekani milioni 348 kupitia mashirika mbalimbali ikiwemo UNICEF, UNESCO na Swedish Development Agency (SIDA) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya elimu.

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania, Martha Makala ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na wadau wa elimu kutoka ndani na nje nchi kwa kuwezesha Kongamani hilo na kuwa uwepo wa watunga sera katika Kongamano hilo utasaidia kufanya mijadala kuwa yenye tija itakayoleta matokeo chanya katika sekta ya elimu. 








Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...