▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira wezeshi ya biashara ▪️Aitaka Kampuni ya Faru Kutoa Kipaumbele cha Ajira kwa wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi, ▪️Ni Uwekezaji wa zaidi ya Tsh Trilioni 1.3. ▪️Serikali kuvuna zaidi ya shilingi trilioni 7 kama mapato. ▪️Ni Mradi Mkubwa zaidi kuwahi kutokea Mkoa wa Morogoro. 📍 Mahenge, Morogoro. Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Peter Mavunde (MB), amezindua rasmi shughuli za ujenzi wa mgodi wa madini ya Kinywe(Graphite), unaotekelezwa na kampuni ya Faru Graphite Corporation kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania (hisa 16%) na Black Rock Mining Limited (hisa 84%) ikiwa ni hatua kubwa katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya sekta ya madini nchini. Akizungumza katika hafla iliyofanyika leo tarehe 9 Oktoba 2025 katika eneo la Mahenge, Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro, Mhe. Mavunde amesema uzinduzi huo ni ishara ya kasi mpya ya uendelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati katika Sekta ya Madini, kutokana na maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Sa...
Marato tv - Sauti ya Jamii