Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wasira:Atahadharisa Watu Wachache Kutumia Mitandao kuleta chokochoko


*Amesema ni kikundi cha watu wachache* *wasioridhika*

*Ataka wananchi wasiwasikilize, waendeleze umoja, mshikamano*

*Amhakikishia Dk. Samia mamilioni ya Watanzania wanamuunga mkono*


Na Mwandishi Wetu,  BUNDA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, ametoa tahadhari kwa wananchi dhidi ya kikundi cha watu wachache wanaoleta chokochoko katika mitandao ya kijamii.

Amesema kikundi hicho ni miongoni mwa watu wachache wasioridhika, hata hivyo kamwe hawatotimiza dhamira yao ovu.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni za urais uliohutubiwa na Mgombea Urais kupitia CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan, mjini Bunda, alisema amani na utulivu utaendelea kutawala nchini.

"Zipo chokochoko nyingi ambazo hazipo kwa watu, zipo kwa wacheche wanaotumia mitandao ya kijamii. Naomba msome ile mitandao kwa makini sana. Kuna watu hawaridhiki.

"Kinamama wanaopika maharage wanafahamu yapo maharage hata ukiyapika vipi yatatokea machache yakielea. Hayo hayaivi na ndiyo watu wanaosumbua," alisisitiza.

Aliongeza: "Watu hao hawawezi kuisumbua nchi, namwambia mgombea wetu (Dk. Samia) asibabaishwe na watu hao wachache, hata ukifanya vizuri namna gani wao wananuna, ndivyo walivyo."

"Wapo watakaokumbuka kwa wema wenye nia njema. Dk. Samia amefanyakazi kubwa, jinsi mnavyomuunga mkono hapa ndivyo anavyoungwa mkono Tanzania nzima," alieleza.

Wasira alisema CCM imewaletea mgombea urais mwenye mafanikio makubwa ya utekelezaji ilani ya uchaguzi iliyopita na siyo mwenye uwezo mdogo.

"Hatuwaletei mgombea urais 'lena' tunawaletea mgombea urais aliye fanyakazi ya urais kwa mafanikio makubwa," alisisitiza.

Alisema Dk. Samia aliingia madarakani katika misukosuko mikubwa wakati ambao taifa lilikumbwa na ugonjwa wa Uviko-19, kufariki dunia kwa Rais aliyekuwa madarakani (Hayati Dk. John Magufuli)  na kushuka kwa uchumi.

Alieleza kuwa, Dk. Samia alipoingia madarakani alitumia maneno mawili ambayo ni 'Kazi Iendelee'.

"Alipewa mtihani mkubwa aliachiwa miradi mikubwa ya nchi yetu. Aliachiwa reli haijakamilika lakini leo imekamilika mpaka Makutupora ya Singida kilometa 722 kutoka Dar es Salaam.

"Aliachiwa bwawa la Mwalimu Nyerere lilikuwa chini ya asilmia 30, hata hivyo asilimia 70 imejengwa chini ya usimamizi wa Rais Samia na Tanzania ina umeme wa kutosha," alibainisha.

Kwa upande wa elimu, Wasira alisema katika Wilaya ya Bunda Dk. Samia amejenga shule mpya 13 za msingi, shule 15 za sekondari, zahanati 20, vituo vitatu vya afya na hospitali moja mpya.

Vilevile, alisema Dk. Samia ametoa mchango mkubwa kupunguza vifo vya kinamama na watoto kwa kuwa alipoingia madarakani alikuta katika kila vizazi hai 100,000 vizazi 500 walifariki dunia kila mwaka.

Alieleza kuwa Dk. Samia amewezesha kushusha hali hiyo ambapo sasa katika kila vizazi hai 100,000  mia tano walikuwa wakifarkki leo vimeshuka kufikia 100.

Awali, Mgombea Ubunge Jimbo la Pangani, Jumaa Aweso, alisema alipokabidhiwa Wizara ya Maji, alipewa maagizo na Dk. Samia kuhakikisha hakuna mwanamke atakayeteseka kwa kukosa maji.

Alisema hali ya maji miaka minne iliyopita katika wilaya hiyo ilikuwa mbaya kwa kuwa miradi iligeuka kichaka cha watu kufanya ubadhirifu.

Aweso alisema Dk. Samia alimwagiza kufika wilayani Bunda kuchukua hatua dhidi ya vitendo hivyo huku akitoa sh. bilioni 10 kutekeleza mradi wa maji Nyabeho.

Alisema mradi huo umeshakamilika, wananchi wanapata maji safi na salama.

"Hapa tuna miradi mingi ambayo ipo ilikamilika na mengine ipo hatua mbalimbali kwa gharama ya sh. bilioni 20. Zaidi ya wananchi asilimia 87 eneo la Bunda Mjini wanapata huduma ya maji," alieleza.

Alieleza kuwa maeneo yaliyokuwa na changamoto ya maji ni vijijini ambapo Dk. Samia amechukua hatua kuhakikisha huduma hiyo inapatikana.

Waziri huyo alisema Dk. Samia ametoa fedha zaidi ya sh. bilioni 100 kutoa maji Ziwa Victoria kwenda Bunda na Tarime.



Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...