Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma
Mwitikio mzuri wa wazazi na walezi kwa kushiriki na kuhakikisha watoto wanapata chanjo ya Polio yapaisha lengo watoto 222,076 Wilaya ya Musoma mkoani Mara wafikiwa.
Wilaya mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amewapongeza wazazi na walezi kwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la utoaji Chanjo kwa watoto.
Amesema katika halmashauri ya Manispaa ya Musoma idadi tarajiwa ilikuwa ni Walengwa 66,176 kutokana na mwitikio mkubwa imepelekea waliopata chanjo hiyo kufikia 77,104 sawa na 120% huku halmashauri ya Musoma Vijijini walengwa walikuwa ni 118,760 na kufikia waliochanjwa 144,972 sawa na 157%.
Nae Mratibu wa Halmashauri ya Musoma DC Joseph Chacha amesema zoezi hilo limefanyika vizuri kutokana na elimu na hamasa iliyotolewa kwa wakati kwa jamii kupitia wenyeviti wa mitaa,vitongoji na vijiji na makundi mbalimbali ya kijamii.
"Ushirikiano katika ngazi zote umeleta matokeo na mwitikio mkubwa kwa jamii na kupata Idadi kubwa ya watoto kupata Chanjo", amesema Joseph.
Jamila Hassan amewapongeza wazazi na walezi kwa kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo ya kuwakinga dhidi ya kupooza ghafla.
"Tunashukuru wote waliohakikisha zoezi hili limefanikiwa na kutekelezwa kwa ustadi mkubwa na kuwezesha kuvuka lengo ambapo utekelezaji umefanyika zaidi ya asilimia".
Kwa mara ya mwisho Tanzania ilipata mgonjwa wa Polio mwezi Julai,1996 ili kulinda afya ya jamii wakati wote Serikali imeiwekea utaratibu wa kufanya ufuatiliaji wa mwenendo wa magonjwa mbalimbali ikiwemo yanayozuilika kwa chanjo kama vile polio.
Katika jitihada hizo za ufuatiliaji magonjwa zilibaini uwepo wa vijidudu vya Polio katika mazingira hasa kwenye sampuli za majitaka jijini Mwanza mwaka 2025 na mwanzoni mwa 2026.
Kutokana na kubainika kwa vijidudu vya Polio katika sampuli za mazingira na uwepo wa tishio la ugonjwa huu kutoka mataifa ya nje Serikali ilifanya maamuzi ya kutekeleza zoezi maalum la kampeni ya chanjo ya Polio ya matone ili kudhibiti na kuzuia ugonjwa huo hapa nchini kwa kuzingatia miongozo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo awamu ya kwanza ilihusisha mikoa ya Mwanza,Geita,Mara,Shinyanga,Simiyu,na Tabora Machi 24 hadi 27,2026.



Comments
Post a Comment