Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Wadau wa maendeleo mkoani Tanga wameipongeza serikali kwa kuelekeza miradi ya kimkakati katika mkoa huu na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hizi zinazokuja.
Wito huo umetolewa na meneja masoko wa Tanga Beach Resort and SPA Firoz Talib alipokuwa akiongea na waandshi wa habari kufuatia uwepo wa miradi mkoani humo ikiwemo ujio wa Bomba la mafuta ghafi linaloendelea kujengwa huko Chongoleani.
Firoz amesema kuwa kutokana na Tanga kusifika katika suala zima la mapishi hivyo basi ni vema wanawake wakachangamkia fursa hiyo kwani imekuja nyumbani na ndio muda wa wao kutamba na kuonesha ujuzi wao kwa wageni wanaokuja.
Aidha Firoz pia ameongeza kuwa ujio huo wa miradi Tanga umewapa hamasa kubwa katika maendeleo kwani hapo awali walikuwa na vyumba vya kulala vichache sana lakini kwasasa wamejipanga kuendana na kasi ya maendeleo iliyopo.
"Ujio wa Bomba la Mafuta Tanga na miradi mingine imepelekea ongezeko kubwa la wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani hivyo basi sisi kama hotel pekee yenye hadhi ya nyota nne tumelazimika kufanya maboresho makubwa ili kuweza kukidhi mahitaji ya wageni hao,awali tulikuwa na vyomba vya kulala 49 lakini baada ya kupata taarifa ya ujio huu wa fursa tumelazimika kufanya maboresho na mpaka sasa tuna vyumba. 118", alisema feroz.
Firoz amemalizia kwa kuwakaribisha wawekezaji wengine kujitokeza kujenga mahoteli na sehemu za kupumzikia kwani kunakoelekea ushindani utakuwa mkubwa na pamoja na uhitaji wa huduma bora.

Comments
Post a Comment