WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi, ameitaka mikoa 13 iliyopewa tahadhari kujiandaa mapema kukabiliana na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua za El Niño.
Akizungumza kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El Niño, Prof. Kabudi amesema mikoa hiyo inapaswa kuhakikisha maandalizi yanafanyika kwa wakati ili kupunguza madhara kwa wananchi na mali zao.
Mikoa iliyotajwa ni Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu,Morogoro, Kigoma, Tanga, Pwani, Ruvuma, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Dar es Salaam.
Prof. Kabudi pia amesisitiza umuhimu wa wananchi kupata na kuzingatia taarifa za tahadhari zinazotolewa na mamlaka husika, huku akivitaka vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa maandalizi na hatua za kuchukua.
Amesema Serikali, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, inaendelea kuratibu maandalizi kwa kushirikisha serikali za mikoa, serikali za mitaa na jamii ili kuhakikisha nchi inakuwa tayari kukabiliana na athari za El Niño.
Ameongeza kuwa ushirikiano wa Serikali na wananchi ni muhimu katika kuzuia athari kubwa na kulinda maisha pamoja na mali za wananchi.
wananchi wametakiwa kuendelea kufuatilia taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na TMA na kutoa taarifa kwa mamlaka husika kwa wakati pindi maafa yanapotokea.





Comments
Post a Comment