Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde, amekutana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mheshimiwa Marianne Young, jijini Dodoma, ambapo wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya madini na kuongeza fursa za uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili kwa kina maeneo ya uwekezaji katika sekta ya madini, uongezaji wa thamani ya madini nchini, pamoja na namna ya kuhakikisha rasilimali hizo zinaendelea kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi jumuishi na wenye manufaa kwa wananchi.
Mkutano huo pia umeangazia umuhimu wa kuendeleza mazingira yatakayowezesha ushirikiano na uwekezaji wenye tija katika sekta ya madini, huku Tanzania ikiendelea kutumia rasilimali zake za madini kama fursa ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Tanzania na Uingereza zimeeleza dhamira ya kuendelea kushirikiana katika maeneo yenye manufaa kwa pande zote mbili, kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya nchi hizo na kukuza ustawi na maendeleo ya wananchi wa mataifa yote mawili.







Comments
Post a Comment