Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imefanya kikao cha maandalizi kwa lengo la kupitia na kuratibu hatua mbalimbali za utekelezaji kuelekea Tamasha la Nne la Utamaduni la Kitaifa, litakalofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 29 Agosti 2026.
Kikao hicho kimefanyika leo, Julai 23, 2026, katika Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika, jijini Dar es Salaam, kikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Methusela Ntonda.
Akiongoza kikao hicho, Bw. Ntonda amesisitiza umuhimu wa ushirikiano na maandalizi madhubuti ili kuhakikisha Tamasha la Nne la Utamaduni la Kitaifa linafanyika kwa mafanikio na kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuenzi utamaduni wa Tanzania.
Kikao hicho kimewakutanisha viongozi na watendaji wa Wizara kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji, ikiwemo uratibu wa shughuli za tamasha, maandalizi, pamoja na mikakati ya kuhakikisha tamasha hilo linafanyika kwa ufanisi.











Comments
Post a Comment