Na. Mohammed Ulongo Katika kutambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari nchini, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), zimetangaza kuwa jumla ya kazi 294 zimefuzu hatua ya mwisho ya Tuzo za Uandishi wa Habari na Makala za Maendeleo za Samia Kalamu Awards 2026. Akizungumza leo Septemba 3, 2026 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Samia Kalamu Awards 2026, Mhandisi Peter P. Mwasalyanda, amesema mkutano huo na waandishi wa habari ulikuwa na lengo la kuwaeleza wananchi namna ya kushiriki katika zoezi la kupiga kura kwa ajili ya kuwapata washindi wa tuzo hizo. Mhandisi Mwasalyanda amesema katika hatua za awali, waandaaji walipokea jumla ya kazi 3,003 zilizowasilishwa na waombaji 985 kutoka maeneo mbalimbali nchini, ambapo baada ya kupitia mchakato wa tathmini, majaji walifanikiwa kuteua kazi 294 ambazo sasa zimefika hatua ya kupigiwa kura na wananchi. Amesema zoezi l...
Marato tv - Sauti ya Jamii