Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Shirika la Nyumba Nchini (NHC) limejipanga kuendelea kutoa huduma ya makazi bora kwa wananchi sambamba na kukabiliana na ongezeko la watu kutokana na kasi ya maendeleo na uhitaji uliopo Kwa sasa.
Hayo yamesemwa na meneja wa Shirika la Nyumba 'NHC' mkoa wa Tanga Mhandisi Mussa Kamendu alipokuwa akizungumza na waandshi wa habari ofisini kwake ambapo amesema kuwa kutokana na kasi ya maendeleo inayochangiwa na uwepo wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ikiwepo Maboresho ya Bandari pamoja na ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi.
"Kazi yetu ni kujenga nyumba na kukarabati nyumba ambazo tunazo tayari,kwahiyo tumejinga vizuri kukabiliana na ongezeko la watu na ndio maana kuna miradi mingine ya nyumba inaendelea na pia tunashirikiana na sekta binafsi kwani shirika pekee yet hatuwezi kumaliza changamoto hii ya makazi ", alisema Mhandis. Kamendu
Aidha Mhandisi Kamendu amesema mpaka sasa kuna mradi wa nyumba 20 za makazi unaoendelea katika eneo la Mkwakwani ambao unatarajia kukamilika mwakahuu wa fedha,na pia wametenga maeneo ya biashara,benki,supa maketi na maduka kwani ongezeko la watu linaenda sambamba na uhitaji wa huduma.
Amesema kuwa kutokana na ujio wa miradi ya kimkakati Tanga kumekuwa na ongezeko kubwa la wageni kutoka nje ya nchini ambao wana uhitaji wa nyumba za makazi na biashara hivyo kufanya NHC kuendeleza kasi yake ya kutekeleza miradi ili kuendana na kasi ya maendeleo.
Ameeleza kuwa hadi sasa shirika hilo lina zaidi ya wapangaji 900 waliopo kwenye nyumba inazozimiliki ambapo mpaka sasa zinaendelea kukarabatiwa ikiwemo kupakwa rangi, kubadilisha mifumo ya maji na umeme.

Comments
Post a Comment