Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MHE. MWINJUMA AFUNGA MASHINDANO YA 'CRDB NANAUKA CUP 2026'

 MTWARA Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Hamisi Mwinjuma, amehitimisha rasmi mashindano ya soka ya 'CRDB Nanauka Cup 2026' yaliyokuwa sehemu ya tamasha kubwa la Mtwara Festival, huku Naliendele FC ikiibuka kidedea na kutwaa ubingwa.  Katika fainali hiyo ya kusisimua iliyopigwa Julai 18 2026 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara, Naliendele FC iliibuka na ushindi wa mikwaju ya penati dhidi ya Vigaeni FC baada kutoshana nguvu kwa sare ya 1-1 na kufanikiwa kukabidhiwa kombe, medali, na kitita cha shilingi milioni tatu. Vigaeni FC iliyoshika nafasi ya pili iliondoka na medali pamoja na shilingi milioni mbili, huku mshindi wa tatu akijinyakulia shilingi milioni moja.  Mashindano haya yameandaliwa na kuratibiwa na Mbunge wa Mtwara Mjini ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana, Mhe. Dkt. Joel Arthur Nanauka. Akizungumza kwenye hafla hiyo, Naibu Waziri Mwinjuma amewapongeza waandaaji kwa kufikia asilimia 100 ya malengo yao, h...

WAZIRI MKUU MWIGULU NA UWT WASHIRIKIANA KUCHANGISHA FEDHA ZA MATIBABU BMH

 NA: MWANDISHI WETU, DODOMA Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, ameshiriki hafla iliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwezesha Mfuko wa Gharama za Matibabu kwa Wagonjwa wa Figo na Upandikizaji Uloto katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH). Hafla hiyo imefanyika Julai 16, 2026, katika Ukumbi wa Mabele Mabeyo Jijini Dodoma, ambapo Dk. Mwigulu amesema, jambo hilo ni jema kwani linawezesha kuokoa maisha ya wagonjwa wengi hasa wasio na uwezo wa kugharamia matibabu hayo. "Tunachokifanya leo ni kurejesha matumaini kwa wagonjwa na familia zao. Kila anayeguswa na jambo hili aendelee kushiriki ili wananchi wengi zaidi wanufaike na huduma hizi muhimu," amesema Dk. Mwigulu. Aidha, amesema serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwekeza fedha nyingi ili kuboresha sekta ya afya kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora. Naye, Wazi wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesema, dhamira ya serikali ni kuhakikisha Tanzania inakuw...

SPIKA ZUNGU AILEZA DUNIA HATUA ZINAZOCHUKULIWA KUCHOCHEA MATUMIZI YA MAGARI YA UMEME NA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

 New York, Marekani Spika wa Bunge Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb) amesema Bunge la Tanzania limechukua hatua madhubuti za kuhimiza matumizi ya magari ya umeme pamoja na gesi. Amesema hatua hizo zimelenga kuimarisha utekelezaji wa mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Mheshimiwa Spika ameyasema hayo leo Julai 14, 2026 wakati akiwasilisha taarifa ya Bunge la Tanzania kuhusu matumizi ya Nishati Safi kwenye  Jukwaa la Kibunge katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (HLPF) 2026. Mkutano huo umefanyika  katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), jijini New York, nchini Marekani. Amesema Bunge la Tanzania limepitisha marekebisho ya sera na sheria za kodi yaliyopunguza ushuru wa magari ya umeme kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 na kwamba misamaha mbalimbali ya ushuru na kodi kwa baadhi ya magari yanayotumia umeme na gesi imetolewa ili kuongeza matumizi ya usafiri r...

CP. KAVIRONDO ASHIRIKI MKUTANO WA 28 WA KAMATI YA MAWAZIRI WA SADC KUHUSU SIASA, ULINZI NA USALAMA

 Na. Ssgt. Mawazo Mtondo - DODOMA Kamishna wa Huduma za Urekebu wa Jeshi la Magereza, CP Amina Kavirondo, akimuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Magereza, CGP Jeremiah Yoram Katungu, alishiriki katika ujumbe wa Tanzania uliohudhuria Mkutano wa 28 wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliohitimishwa Julai 18, 2026, mjini Salima, Malawi. Ushiriki wa Kamishna wa Huduma za Urekebu katika mkutano huo unaonesha mchango wa Jeshi la Magereza katika masuala ya usalama wa Taifa na ushirikiano wa kikanda, sambamba na dhamira ya Tanzania ya kuimarisha amani, ulinzi na usalama ndani ya nchi na katika ukanda wa SADC. Tanzania, ikiwa ni miongoni mwa nchi waasisi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ilishiriki kikamilifu katika Mkutano huo ambao ulianza kwa vikao vya ngazi ya Makatibu Wakuu vilivyofanyika Julai 13 na 14, 2026, na kufuatiwa na vikao vya ngazi ya Mawaziri vilivyofanyika Julai 16 na 17, 2026. Katika ngazi ya...

PROFESA TIBAIJUKA AIPONGEZA ST ANNE MARIE KWA MIAKA 25 ILIYOSHEHENI MAFANIKIO

 Na Mwandishi Wetu Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka amewataka wakaguzi wa shule kutenda haki kwa shule binafsi na kuziona kama mshirika wa maendeleo badala ya mshindani. Kadhalika, Profesa Tibaijuka ameipongeza shule ya St Anne Marie Academy kwa kuendelea kusomesha bure wanafunzi wanaofiwa na wazazi wao ikiwa shule pekee ya binafsi inayofanya hivyo kwa sasa nchini. Alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa shule hiyo Julai 18 mwaka 2001. Aliwataka wakaguzi wa elimu nchini kuacha kuziwekea vikwazo shule binafsi kwa kuziona kama washindani kwenye sekta ya elimu na badala yake wanatakiwa kuwaona kama washirika muhimu kwenye kutoa huduma hiyo. ”Unakuta wanawawekea wenye shule binafsi viwango vya kusadikika tofauti kabisa na shule za umma, sisemi kwama muwawekee viwango hafifu, hapana mimi nataka uwiano wa haki baina ya shule za umma na shule binafsi,” alisema Alisema sh...

DC ITUNDA AWATUNUKU VYETI WAHITIMU 70 KAPS MBEYA, AWAPA NENO ZITO KUJIAJIRI

 Na Mwandishi Wetu, Mbeya MKUU wa Wilaya ya Mbeya, Mhe. Solomon Itunda, amewatunuku vyeti wahitimu 70 wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (KAPS) na kuwataka kutumia elimu waliyoipata kuwa chachu ya mabadiliko chanya na kutengeneza fursa za kujiajiri badala ya kusubiri ajira za kuajiriwa. Hafla hiyo ya mahafali imefanyika Julai 17, 2026, katika viwanja vya chuo hicho kilichopo mtaa wa Forest, Jijini Mbeya, ambapo wahitimu hao walihitimisha masomo yao na kutunukiwa Astashahada (Certificate) ya Maendeleo ya Jamii. Akizungumza wakati wa hafla hiyo akiwa kama Mgeni Rasmi, Mhe. Itunda aliwapongeza wahitimu hao kwa juhudi, nidhamu na uvumilivu waliouonesha katika kipindi chote cha masomo yao, na kuwakumbusha kuwa maendeleo ya Taifa yanategemea nguvu kazi yenye maarifa na uzalendo. "Mnapaswa kwenda kuwa chachu ya maendeleo katika maeneo yenu kwa kuzingatia misingi ya kazi na utu. Tumieni elimu mliyoipata hapa kujiajiri na kuajiri wengine, huku mkizingatia maadili ya kazi, uzalendo na uwajibika...