Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

HOTUBA YA RAIS SAMIA URUSI NI USHINDI KIUCHUMI, KIJAMII, NA KIDIPLOMASIA!


Na Beda Msimbe,TBN, aliyekuwa Urusi

IJUMAA Juni 5, 2026 ilikuwa siku ya kihistoria na ya kipekee, wakati Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alisipomama mbele ya viongozi wa dunia katika Jukwaa la Kimataifa la Uchumi (St. Petersburg International Economic Forum) na hoja nzito zenye mashiko, akibeba sauti ya Watanzania wote na kuweka wazi fursa zinazopatyikana Tanzania ikiwa na pamoja na mwelekeo mpya wa nchi katika kutengeneza uchumi wa kisasa.

Jukwaa hilo lilikuwa sehemu muhimu ya ziara ya Rais Samia ambayo haikuwa tu ya itifaki, bali ya kueleza milango wazi ya fursa za kiuchumi na kijamii.

Jinsi Rais Samia alivyopokewa na kukirimiwa nchini Urusi katika shughuli zoye zilizomhusu, ilionesha taswira ya urafiki wa dhati na cheko tupu kati yake na mwenyeji wake, Rais Vladimir Putin. Ziara hiyo ilirudisha historia, ikaweka wazi haja ya sasa baada ya ukombozi wa kisiasa kusaidiana kupatikana kwa ukombozi wa kiuchumi na ustawi wa jamii zote mbili.

Akiwa katika jukwaa la kiuchumi, akizungumza na washiriki hotuba ya Rais Samia iliwatafakarisha wahusika, kwani ilkijaa hoja za uchambuzi wa kina na haja ya dunia kubadilika

Rais Samia alifanya uchokozi wa fikira na moja ya uchokozi huo alisema bila kupepesa kuwa ifikapo mwaka 2050, mtu mmoja kati ya wanne duniani atakuwa Mwafrika; na takwimu hizo kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ziliambatana na swali: "Je, Afrika itastawi na kukuaa kwa masharti ya nani, na kwa modeli ya nani ya uchumi?" 

Swali hilo lenye mantiki kubwa liliulizwa kwa shauku kubwa kutokana na siasa za kijiopiti ambazo zimekuwa zikiyumbisha ushirika wa kawaida na kujazwa na masharti ya kuangushana na kudhibitiana katika mfumo ambao unamlazimisha maskini asiendelee au kuchaguliwa patna wa kuzungumza naye.

Katika misingi mikubwa ya kufikiri kilojiki Rais Samia alikuwa anaitafadhalisha dunia sio kuistiri Afrika bali kutambua ukweli na kuiacha Afrika ijiamulie mambo yake yenyewe.

Mathalani Afrika kwa sasa ina Ajenda 2063 na soko la AfCFTA, lakini kuna mataifa yanayoendelea kuingilia kati kila mara na kuwatenganisha waafrika ili wajifikirie wanahitaji masaada katika utatuzi wa kero zinazowakabili. 

Rais Putin aliunga mkono hoja hiyo, jambo lililoleta miguno ya ridhaa na vigelegele ukumbini.Kuna mambo mengi yanayopaswa kufanywa na Waafrika wenyewe yenye manufaa makubwa kwa binadamu. 

Mambo yaliyoguswa

Katika hotuba yake na ziara hiyoik ya Urusi Rais Samia amegusa mambo mengi. Hapa tunaweza kuangazia maeneo makubwa yaliyoguswa na jinsi makubaliano yalivyomalizika ikiwa ni mafanikio makubwa kwa Tanzania.

Ikumbukwe kwamba ndani ya ziara ya Rais Samia ambapo pia aliambatana na wafanyabiashara inakumbusha ulimwengu kuhusu mizizi imara ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Urusi. Kuna historia ndefu ya mahusiano kuanzia miaka ya uhuru,kwani siku mbili baada ya Tanzania bara kupata uhuru, Urusi ilituma salamu vivyo hivyo kwenye mapinduzi matukufu ya Zanzibar.

Mbele ya wawekezaji, Rais Samia alibainisha kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi ya takribani 6%, ukiwa miongoni mwa chumi zinazochangamka zaidi Afrika. 

Alitangaza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kumfikisha kila Mtanzania kwenye kipato cha wastani cha dola $7,000$ huku akielezea fursa za uwekezaji na biashara nchini Tanzania

Hotuba yake hiyo iliyopigiwa makofi mara kwa mara iliwavutia matajiri wa Kirusi, ambapo sekta binafsi ya Urusi ilikiri kuwa Tanzania ni soko salama na lenye utulivu wa kisiasa unaoruhusu ukuaji wa mitaji.

Lakini hayo yamesemwa wakati pia Rais akieleza kuwapo kwa Mapinduzi makubwa ya Miundombinu (Reli na Bandari). Rais Samia ambaye katika mkutano huo pamoja na ule wa pembeni ambapo wafanyabiashara wa Tanzania walipata nafasi ya kuzungumza na wenzao wa Urusi, alieleza kwa kina ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) inayounganisha Bandari ya Dar es Salaam na nchi za Rwanda, Burundi, na DRC na faida yake kwa wakazi wa eneo hili. 

Pia alitaja mpango wa miaka mitano (2026–2031) wa kupanua reli hiyo hadi Musoma, na kuunganisha ukanda wa kusini kuelekea Malawi na Msumbiji. Urusi ikiwa na uzoefu mkubwa wa teknolojia ya reli na usafirishaji, ilionesha nia ya kutoa utaalamu wa kihandisi na mitambo ili kuharakisha uunganishaji wa reli hizo za kikanda.

Suala la kuwepo kwa maboresho ya uwekezaji na mifumo ya saa 24 kulileta msisimko mkubwa. Rais alieleza jinsi uwekezaji ulivyopaa kutoka dola bilioni 3 (2021) hadi dola bilioni 12 (2025) kutokana na mfumo wa usajili wa kampuni unaochukua hadi saa 24 tu. Ni kutokana na kutambulika kwa ukweli huu Taasisi za uwekezaji za Tanzania (TIC) na zile za Urusi zilisaini mikataba ya ushirikiano. Hatua hii ilifungwa kwa cheko na bashasha, kwani urasimu sasa umepigwa marufuku rasmi.

Aidha Miradi ya Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo na Bandari ya Kimataifa ya Mizigo ya Mangapwani (Zanzibar) ilipewa kipaumbele cha juu na makampuni makubwa ya Urusi yanayohusika na masuala ya meli na usafirishaji wa baharini. Wao walikubali kutuma timu za wataalamu nchini Tanzania kufanya upembuzi yakinifu wa namna ya kuwekeza kwenye bandari hizo.

Kwenye Sekta ya Madini Rais Samia alizungumzia haja ya Tanzania ambayo ni Kuongeza Thamani Ndani ya Nchi.Tanzania ikiwa na utajiri wa dhahabu, uranium, nickel, graphite, helium, na madini adimu.

"Hatutaki tena kuuza malighafi pekee, tunataka viwanda vya usindikaji hapa nchini."alisema Rais Samia. Urusi, ikiwa ni mbabe wa madini, ilimalizia haja ya Tanzania kwa kukubali kujenga viwanda (Industrial Parks) nchini Tanzania ili kuchenjua na kuongeza thamani ya madini kabla hayajasafirishwa kwenda nje.

Katikia ziara hii Rais Samia alielezea na kudhihirisha ni kwa namna gani Tanzania iko tayari kwa biashara, ubunifu, na ushirikiano wa kufanikisha kila hatua itakayochangia ustawi wa wananchi wake.

Wakati Rais Samia akimaliza hotuba yake kwenye jukwaa hilo la St Petersburg kwa kutoa shukrani za dhati kwa Rais Vladimir Putin kwa ukarimu wake, viongozi hao wawili walionesha tabasamu la furaha, ikiwa ni ishara ya kukubalika kwa hoja za Tanzania na mwanzo mpya wa dhahabu katika uhusiano wa mataifa haya mawili. 



Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...