Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 01 Septemba, 2026, anaondoka nchini kuelekea Lusaka, Zambia kuhudhuria sherehe za Uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Zambia, Mheshimiwa Hakainde Hichilema.
Katika Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika tarehe 13 Agosti, 2026, Rais Hichilema alichaguliwa kuiongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano.
Ziara ya Rais Dkt. Samia inaendeleza uhusiano wa kindugu na kihistoria kati ya Tanzania na Zambia, unaojengwa katika misingi ya umoja, mshikamano, ujirani mwema na ushirikiano wa kikanda.

Comments
Post a Comment