Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

MWENGE WA UHURU 2026: MAKUNDI MAALUMU YAPONGEZWA MULEBA, WANANCHI 690 WANUFAIKA MRADI WA MAJI

 Na Angela Sebastian, Kagera KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’onda, amepongeza ushiriki wa makundi maalumu katika mbio hizo wilayani Muleba, mkoani Kagera, akisema hatua hiyo ni ishara kuwa Mwenge wa Uhuru ni mali ya wananchi wote bila kujali hali zao katika jamii. Mwang’onda alitoa kauli hiyo jana wakati wa ziara ya Mwenge huo wilayani Muleba, ambapo alieleza kufurahishwa na namna makundi hayo yalivyoshiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za mbio hizo. Alisema ushiriki huo unaakisi umoja, mshikamano na jitihada za Serikali za kuwahusisha wananchi katika shughuli za maendeleo. Katika hatua hiyo, Mwang’onda akiwa na Wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, aliwakabidhi Mwenge huo makundi maalumu na kushiriki nao katika shughuli mbalimbali, jambo lililowapa furaha na kuifanya mbio hiyo kuwa jukwaa la wananchi wote. Alisema kwa sasa Mwenge umekabidhiwa kwa wananchi, hivyo ni muhimu kila kundi kushiriki katika kuunga mkono juhudi za kuleta mae...

CHATANDA: NDEJEMBI ANA UWEZO MKUBWA WA KUMSAIDIA MAJUKUMU RAIS WETU

NA: MWANDISHI WETU, DODOMA Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, ameelezwa kuwa kiongozi mahiri, muadilifu na mzalendo, mwenye uwezo wa kumsaidia majukumu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Mary Chatanda, Agosti 30, 2026, ofisini kwake Dodoma, siku moja baada ya kukamilika uapisho wa kiongozi huyo, Ikulu ya Chamwino, Dodoma. Chatanda ameeleza, Ndejembi ni kiongozi wa vitendo na katika majukumu aliyoaminiwa tangu akiwa Mkuu wa wilaya ya Kongwa, Mbunge, Naibu Waziri na Waziri kamili katika wizara mbalimbali. "Kule Kongwa Dodoma akiwa Mkuu wa wilaya alifanya kazi nzuri na katika kilimo alisimamia kwa mafanikio makubwa kampeni yake aliyoiita ONJAKO yaani Ondoa Njaa Kongwa. Alihimiza wananchi kulima mazao yanayostahimili ukame kama mtama, mihogo, ufuta na alizeti ili kuwaepusha wananchi na kadhia ya njaa," amesema Chatanda. Ameongeza kuwa, kampeni ya ONJAKO ilipokelewa vizuri na wakulima wa Kongwa kut...

ELIMU NA HAMASA NZURI YAWAFANYA WAZAZI NA WALEZI KATA YA MWISENGE KUHAKIKISHA WATOTO WAO WANAPATA CHANJO YA POLIO.

Na Mwandishi wetu Jovina Massano Musoma. ELIMU na hamasa nzuri kwa jamii yasababisha wazazi,watoto na walezi  Kata ya Mwisenge Manispaa ya Musoma mkoani Mara kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo ya Polio awamu ya tatu. Hayo yamesemwa na wazazi na walezi Agosti 30, 2026 katika mitaa na maeneo ya Ibada mara baada ya kufikiwa na timu ya utoaji chanjo. Wamesema kuwa wahamasishaji wakiwemo wenyeviti wa mitaa na taarifa zinazotolewa katika vyombo vya habari zimewafanya wamepata hamasa na uelewa mpana wa umuhimu wa chanjo hiyo. Wakizungumza kwa  Nyakati tofauti wamesema utoaji elimu mapema ni muhimu kwa kuwa inasaidia kupata taarifa na uelewa usahihi wa zoezi husika. Frank David afisa usafirishaji wa Mtakuja Kituo Cha mianzini ni miongoni mwa wazazi ambae nae mtoto wake ameweza kupata chanjo hiyo. Amesema hapo awali watu waliongea vibaya kuhusiana na chanjo ya Polio wengi walipata hofu lakini hivi sasa baada ya kupewa elimu kwa usahihi  imewapa ujasiri wa kuhakikisha watoto wa...

DKT. MWIGULU AWASILI KATAVI KUSHIRIKI JUBILEI YA MIAKA 25 YA JIMBO KATOLIKI LA MPANDA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Agosti 30, 2026, amewasili Mpanda mkoani Katavi kuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 25 ya Jimbo Katoliki la Mpanda. Maadhimisho hayo yanafanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari St. Mary, Mpanda, mkoani Katavi.

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MISA YA IBADA TAKATIFU KANISA KATOLIKI DODOMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi, pamoja na familia yake wameungana na waumini mbalimbali katika kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Jumapili, katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu Katoliki Dodoma. Tarehe 30 Agosti 2026.

SILLO:MICHEZO,BURUDANI NI NGUZO YA AFYA YA AKILI NA UFANISI KAZINI

 NAIBU Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Daniel Sillo, amesema michezo na burudani ni nguzo muhimu katika kupunguza msongo wa mawazo, kuimarisha utimamu wa akili na kuongeza ufanisi katika kazi. Mhe. Sillo ameyasema hayo jana Agosti 29, 2026, wakati wa tamasha la NMB Bunge Bonanza lililofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlini jijini Dodoma, likiwakutanisha zaidi ya washiriki 1,000 kutoka Bungeni, Wizara 14 na Taasisi 10, wakiwemo wadau na wadhamini wa tamasha hilo. Bonanza hilo lililobeba kaulimbiu “Pamoja AFCON 2027: Tanzania Tupo Tayari”, limeelezwa kuwa si tu fursa ya kufanya mazoezi na kujenga afya, bali pia ni jukwaa la kuimarisha mshikamano, kufahamiana na kujenga umoja miongoni mwa watumishi na viongozi kutoka taasisi mbalimbali. “Michezo ni fursa ya kipekee inayotuwezesha kufahamiana, kujenga mshikamano na kuimarisha umoja wetu. Bunge lipo tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha michuano ya AFCON 2027 inafanyika kwa ubora wa hali...