Wahitimu wa vyuo vya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi nchini Tanzania wanatarajiwa kuwa na ujuzi unaoendana zaidi na mahitaji ya soko la ajira, kufuatia hatua inayochukuliwa kupitia Mradi wa ESPJII wa kuandaa viwango vya Kazi. Mradi huo unalenga kukuza viwango vya ujuzi nchini kwa kuimarisha mifumo ya mafunzo, kuwajengea uwezo walimu pamoja na kuboresha matumizi ya teknolojia katika sekta ya TVET. Akizungumza kuhusu mchakato huo leo Agosti 27,2026 Mratibu wa Mradi huo kutoka NACTVET Bw. Aggrey Mleli amesema maandalizi ya miongozo ya Viwango vya kazi ni hatua muhimu katika kuhakikisha mafunzo yanayotolewa katika taasisi za TVET yanaendana na mahitaji halisi ya ulimwengu wa kazi. Mleli amesema kikao cha wadau kilichofanyika ni sehemu ya hatua ya pili ya kupitia na kukusanya maoni kutoka kwa wadau kabla ya miongozo hiyo kupelekwa katika ngazi za juu kwa ajili ya kuidhinishwa na kuanza kutumika katika maandalizi ya kuandaa viwango vya Kazi. Amesema mchakato huo ni muhimu kutokana na mabad...
Marato tv - Sauti ya Jamii