Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

DKT. MWIGULU AAGIZA WALIOIBA MILIONI 500 MANYONI KUKAMATWA

*_▪︎ Aagiza watumishi waliohusika na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 500 Manyoni wakamatwe na fedha zirudishwe_* *_▪︎ Akemea rushwa, wizi wa fedha za umma na matumizi mabaya ya madaraka_* *_▪︎ Aonya viongozi wanaowaza vyeo badala ya kutatua changamoto za wananchi_* WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameagiza watumishi waliohusishwa na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 500 katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni watafutwe popote walipo, wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria na kinidhamu huku fedha hizo zikirejeshwa serikalini. "Wamechota fedha za wananchi. Watafutwe hata ambao walishahamishwa, popote walipo wakamatwe, wawekwe ndani na fedha za Serikali zirudi. Hii si fedha ya mtu binafsi, ni fedha ya wananchi," alisema Dkt. Mwigulu. Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo Jumamosi Mei 30, 2026 alipozungumza na wananchi wa Wilaya ya Manyoni katika Viwanja vya Tambukareli mkoani Singida akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kusi...

SKIMU ZA UMWAGILIAJI ZINAVYOPELEKA FURAHA KWA WAKULIMA MBARALI

Wakulima wa zao la mpunga wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya wameiomba Serikali kuendelea na utekelezaji wa miradi 10 ya skimu za umwagiliaji inayotekelezwa wilayani humo, wakisema tayari imeanza kuleta matokeo chanya katika uzalishaji wa mazao. Wakulima hao wanasema licha ya miradi hiyo kutokukamilika kwa asilimia zote, uzalishaji wa mpunga umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 80 kutokana na upatikanaji wa uhakika wa maji. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakulima hao wameridhishwa na ongezeko la mavuno katika msimu huu na kubainisha kuwa miradi ya Umwagiliaji imekuwa chachu ya maendeleo ya kilimo katika wilaya hiyo. Meneja wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mkoa wa Mbeya, mhandisi Banzi Abdallah amesema utekelezaji wa miradi hiyo umefikia asilimia 60 na kwamba hatua mbalimbali zinaendelea kuhakikisha inakamilika kwa wakati ili kuwanufaisha wakulima wengi zaidi. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Raymond Mweli amesema skimu za Umwagiliaji zina mchango mkubwa katika...

WAZIRI MKUU APONGEZA KILIMO CHA KOROSHO MANYONI, AHIMIZA UONGEZAJI THAMANI WA MAZAO KUPITIA VIWANDA

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kukuza uchumi wa viwanda na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, huku akiwataka vijana, sekta binafsi na wawekezaji kutumia fursa zilizopo kuanzisha viwanda vya kuchakata korosho na mazao mengine ya kilimo. “Serikali haipaswi kufanya jukumu hilo peke yake la kujenga viwanda. Lakini kwa kuwa zao hili halikuwa zao la asili lililozoeleka kwa Mkoa wa Singida, ni lazima hatua za aina hii ziweze kufanyika. Baada ya hapo vijana na sekta binafsi wachukue jukumu hilo la kutengeneza viwanda vya kutosha vya kubangua korosho zinazozalishwa hapa Mkoa wa Singida na pengine hata mikoa mingine,” alisema Dkt. Mwigulu. Dkt. Mwigulu amesema hayo leo Jumamosi Mei 30, 2026 alipokagua Mradi wa Mnyororo wa Thamani wa Korosho kupitia Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho (KIDAKUKO) cha CAMARTEC kilichopo Masigati wilayani Manyoni, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Singida. Waziri Mkuu aliwapongeza wananchi wa Manyoni kwa...

WALIOBOMOLEWA NYUMBA, MWANAFA AWAAHIDI WATALIPWA FIDIA

📍 Ni zile familia 67 zilizobomolewa nyumba na Amboni Plantation  Na Mwandishi Wetu, Kigombe MBUNGE wa Muheza, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA), amewahakikishia wananchi wa kaya 67 waliobomolewa nyumba zao na Kampuni ya Amboni Plantation kuwa watalipwa fidia zao kikamilifu. Uharibifu huo wa dharura ulioacha familia hizo za Kitongoji cha Maisha Plus mkoani Tanga zikilala nje, ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwa madai ya wananchi hao kuvamia eneo la shamba la mkonge la mwekezaji huyo. Akizungumza jana Mei 29, 2026 aliporejea kijijini hapo kutoa mrejesho wa kikao chake cha ndani na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, MwanaFA alisema Serikali imejipanga vizuri kulinda utu wa wanyonge hao. "Sitaki kuwaambia ni kiasi gani mtalipwa, lakini sisi kama viongozi wenu tunawahakikishia jambo lenu litakwenda vizuri na mtalipwa fidia kabla ya kuondoka hapa. Suala hili linanikosesha usingizi na sitarudi kwenye majukumu ya kitaifa hadi dharura hii iishe," alisema MwanaFA. M...

TANZANIA YAUNGA MKONO UBUNIFU MPYA KIFEDHA KWA AJILI YA MITADI YA USAFIRI NA AFYA

Na Benny Mwaipaja, Congo Brazzaville Tanzania imeelezea msimamo wake wa kuunga mkono mbinu za fedha za mseto (blended finance) zitakazosaidia kuimarisha sekta za usafiri wa anga na afya barani Afrika, akieleza kwamba hakuna chanzo kimoja kitakachoweza kuziba mapungufu ya miundombinu ya bara hilo. Akizungumza kama Gavana Mbadala wa Tanzania kwenye mkutano ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuhusu “Platform solutions to Africa’s Transformation: De‑risking Aviation and Health systems through Innovative Financing”, jijini Congo Brazzaville, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba alisema suluhisho linalopendekezwa ni la vitendo, nafuu na linaendana na vipaumbele vya kitaifa vya Tanzania. “Tunasisitiza matumizi ya rasilimali za umma na binafsi pamoja na dhamana na msaada kutoka kwa washirika. Hatuwezi kutegemea chanzo kimoja pekee,” alisema Dkt. Mwamba, akiongeza kuwa ni muhimu kuzingatia udhibiti wa deni linalozidi kukua katika n...

UWEPO WA MADUKA YA NYARA HAPA NCHINI UTAIMARISHA USIMAMIZI MADHUBUTI

Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Uimarishaji uhifadhi unazidi kuboreshwa na Serikali ya awamu ya sita kwa kuweza kuanzisha maduka maalum ya kuuza nyara na kuweka historia mpya  tangu Uhuru. Uanzishwaji huo umechukuliwa mara baada ya Machifu kutoka makabila mbalimbali nchini kuiomba Serikali kuwezesha upatikanaji wa nyara kwa makundi yanayohitaji kuzitumia katika mila na desturi. Maombi hayo yaliwasilishwa kwa Mh.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan jijini Mwanza wakati wa tamasha la Bulabo ambalo hufanyika kila Mwaka linalokutanisha Viongozi wa mila na desturi kwa maana ya machifu kutoka mikoa mbalimbali. Katika tamasha hilo waliweza kumsimika Mh.Rais wa awamu ya sita kuwa   Chifu mkuu  na mmiliki wa mila na desturi zilizo njema huku wakimpa jina la Chifu Hangaya. Chifu Hangaya hakusita kuchukua hatua madhubuti kwa kuanzisha maduka hayo  kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) katika mikoa ya Mwanza na Arusha. Umuhimu wa maduka haya yatawezesha usi...