Na Mwanamkuu Mwandoro , Tanga.
MWANAFUNZI wa amali ya upishi kutoka shule ya Sekondari ya wasichana ya Korogwe iliyopo mkoani Tanga Ntuli Danken Mwanganga ameanza kuona mwanga hadi kutamani kutimiza ndoto ya kuwa mfanyabiashara mkubwa wa chakula ujuzi ambao alianza kujifunza kutoka mikononi mwa Mama yake mzazi aliyekuwa mama ntilie akihitaji kuiboresha zaidi biashara hiyo.
Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya kitaifa ya elimu ujuzi na ubunifu yanayoendelea kufanyika kitaifa mkoani Tanga Ntuli ameishukuru mamlaka ya elimu Tanzania (TEA)kwa kuwapatia vifaa ambavyo vimekuwa msaada mkubwa katika kujifunza kwao kwani vimewaongezea uelewa tofauti na awali walipokuwa wakijifunza kwa nadharia pekee.
"Mwanzo wakati hatujaletewa vifaa ilikiwa shida sana kujifunza tulikiwa tunasoma tu na kuelekezwa hata matokeo yetu hayakuwa mazuri lakini sasa tunawashukuru sana TEA kwa kutuletea vifaa tunajifunza kwa vitendo na kutumia vifaa"
"Nimependa na nimechagua somo la upishi kwa sababu wakati ninasoma shule ya mazingira nilikuwa namuona mama yangu akiingiza pesa kila siku kupitia upishi wa supu ndoto yangu nataka nisome nije kuwa mamalishe mkubwa vya kula vyote iwe natengeneza" amesema Ntuli
Ntuli ameitaka jamii kuwa na mtazamo chanya juu ya masomo ya Amali kwa kile kinachoelezwa kuwa wanafunzi wanaosoma amali hawana akili ama wamefeli kumbe ni tofauti kwani sasa tupo katika kipndi cha sayansi na teknolojia hivyo wajuzi na wabunifu wengi wanahitajika.
"Tunaomba wazazi wawashauri watoto wao waende kujifunza masomo ya Amali watu wengi wanasema kwamba wanaosoma Amali ni mtu ambaye hana akili na amefeli mitihani yake.
Ntuli pia amesisitiza umuhimu wa kusoma amali kwani unapomaliza kidato cha nne unapata vyeti viwili ambavyo ni cheti kutoka Baraza la taifa la mitihani (NECTA) na cheti kutoka Chuo Cha ufundi (NACTIVAT),ambavyo vitakuwa vitakurahisishia katika kuendelea mbele na hatua nyingine.
Awali akizungumza Afisa uhusiano na mawasiliano mamlaka ya elimu Tanzania (TEA)Eliafile Solla amesema kuwa milango ya taasisi hiyo Iko wazo kuwakaribiaha wadau mbalimbali wa elimu kutoka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kuja kuwekeza katika sekta hiyo kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ambazo zinalenga kuinua uchumi jumuishi kwa kizazi kijacho.
"Tunahitaji sana tupate mchango wa wadau wa elimu ambao wapo tayari kuchangia sekta ya elimu kupitia mfuko wa elimu wa Taifa na atatambuliwa kwa kutangazwa kitaifa na kimataifa"
Amesema kuwa amamlaka ya elimu Tanzania 'TEA' imeendelea kuweka mazingira rafiki kwa lengo la kujifunza masomo ya amali ambapo mpaka sasa ujumla ya shule 35 zimepatiwa ufadhili wa vifaa vya kujifunzia mkondo wa Amali zikitumika zaidi ya Shilingi Bilioni 6 katika uwekezaji huo.
"Moja kati ya miundombinu ambayo mamlaka ya elimu Tanzania imeipa kipaumbele ni kuboresha miundombinu ya kujifunzia masomo ya Amali mpaka sasa hivi TEA imefanikiwa kuzifikia shule 35 kwa kuzipatia ufadhili wa vifaa vya kujifunzia mkondo wa Amali zaidi ya Bilioni 6 zimetumika kwaajili ya kununulia vifaa hivyo" amesema Solla.
Aidha ameishukuru na kuipongeza Serikali kwa kuendelea kuiwezesha mamlaka hiyo ya elimu Tanzania 'TEA' kupitia fedha ambazo imeziwekeza na zimeendelea kuleta matokeo mazuri kwa jamii hususani wanafunzi ambao ndio walengwa wakuu wakionekana kuwa na mabadiliko baada ya kuanza kujifunza masomo ya Amali kwa vitendo.
Mamlaka ya elimu Tanzania(TEA) inajukumu la kutafuta rasilimali feda na vifaa kwaajili lengo la kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.





Comments
Post a Comment