Na Mwandishi wetu Jovina Massano
Viongozi wa Wilaya na halmashauri ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara washiriki zoezi la utoaji chanjo.
Zoezi hilo limeanza rasmi Agosti 27,2026 na litahitimishwa Agosti 30,2026 ambapo watoa huduma watafanya zoezi hilo nyumba kwa nyumba,mashuleni kwenye masoko,nyumba za Ibada na kwenye maeneo yenye mkusanyiko.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amewatoa hofu na kuwahimiza wazazi na walezi wenye watoto walio chini ya miaka 10 kuwa chanjo hiyo ni salama imekidhi viwango vya kitaifa na kimataifa kwa kuwa imethibitishwa na kuidhinishwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba Tanzania (TMDA) sambamba na Shirika la Afya Duniani (WHO).
"Kampeni ya chanjo ya matone inatekelezwa ili kuhakikisha Jamii inakuwa na kinga kamili dhidi ya ugonjwa wa Polio pia inatolewa bure,haina madhara kwa watoto imethibitishwa na wataalam wa kitaifa na kimataifa Polio ni miongoni mwa magonjwa yanayozuilika,"amesema Chikoka.
Amesisitiza kuwa ni muhimu kuhakikisha walengwa wote katika zoezi hili la chanjo ili kulinda afya ya jamii wakati wote.
Hata hivyo Mratibu wa Chanjo Manispaa ya Musoma Jamila Hassan amebainisha urudiaji wa kampeni hii ni kutokana na kuwepo kwa Idadi kubwa ya watoto ambao hawakufikiwa katika awamu ya kwanza na kuendelea kuwepo kwa tishio la ugonjwa huu katika mataifa ya nje yenye mwingiliano mkubwa na nchi yetu.
Hivyo ni muhimu walengwa wote ambao ni watoto chini ya miaka 10 kwa maana ya walio na miaka 9 na miezi 11 hadi miezi 0 wanapata chanjo ya Polio kwa kinga kamili.
Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Nyambiti amesema Taifa lolote linategemea rasilimali watu lakini watu wenye afya bora kwa kuanza sasa hivi kwa kuwapa Chanjo hizi zinawafanya wao wawe na kinga kubwa ya kuweza kuhimili magonjwa .
Amewaomba wale wote wanaotekeleza zoezi hili kuhakikisha wanapita nyumba kwa nyumba kuwapa watoto chanjo hiyo na amewaomba wananchi waache Imani potofu ya chanjo washiriki kikamilifu kwa afya ya watoto.







Comments
Post a Comment