Hafla ya uapisho imefanyika katika Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma, na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na wageni wengine.
Mhe. Ndejembi ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju, huku Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akishuhudia tukio hilo.
Uapisho huo unamuweka rasmi Mhe. Ndejembi katika nafasi ya Makamu wa Rais, ambapo ataanza kutekeleza majukumu ya kikatiba ya nafasi hiyo kwa kushirikiana na Rais katika kuongoza na kusimamia shughuli za Serikali pamoja na kulitumikia Taifa na wananchi wake.
Hatua hiyo pia inaashiria mwanzo wa awamu mpya ya uongozi kwa Mhe. Ndejembi, akibeba jukumu muhimu la kusaidia Rais katika utekelezaji wa majukumu ya Serikali na kuhakikisha masuala ya maendeleo na ustawi wa Watanzania yanaendelea kupewa kipaumbele.









Comments
Post a Comment