Mwili wa Mhe. Lukuvi ulisafirishwa kutokea Iringa mjini mara baada ya kufanyiwa Ibada Maalum na kuagwa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu Kanisa Kuu - Kihesa, Jimbo Katoliki Iringa leo Machi 30, 2026.
Mhe. Lukuvi alifariki dunia tarehe 25 Machi, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu, anatarajiwa kuzikwa Leo Machi 31, 2026 Kijiji Idodi.
















