Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ameahidi kuwachukulia hatua za kisheria wote wanao kwamisha ajenda ya serikali juu ya matumizi ya stendi ya magufuli huku akisema kuwa Rais Samia hajatuma viongozi kuua stendi hiyo.
Hayo amebainisha leo Agosti 19, 2026, Mkuu wa mkoa huyo katika ziara yake katika wilaya ya Ubungo alipofika katika stendi ya mabasi Magufuli kwa lengo la kuzungumza na wafanyabiashara na madereva katika stendi ya hiyo ambapo amesema wapo badhi ya watumishi wa umma wamekuwa sehemu ya kuhujumu mradi huwo.
Chalamila amesema serikali ipo katika uchunguzi wa biashara haramu ya matumizi na usafurushaji wa madawa ya kulevya kupitia stendi ya maguguli ili kuhakikisha shughuli halamu zinakomeshwa na kuweka mifumo mizuri ya usalama katika mkoa wa Dar es salaam.
Adha Mkuu wa Mkoa ameitaka LATRA kufuta vibali vya magari vyote kwa anaekaidi kutumia stendi ya magufuli ili kuweka mifumo bora ya utii wa sheria na kuongeza mnyororo wa thamani ya biashara kupitia sekta ya usafiri.
Kwa upade wake Mbunge wa Jimbo la Kibamba na Waziri wa Mawasiliano ya habari Angellah Kairuki amewataka wamiliki wa mabasi kutojaribu kuchezea serikali kwa kutoafuata maagizo ya serikali kupitia katazo la Mkuu wa mkoa Albert Chalamila la kupiga marufuku maegesho ya mabasi katika eneo la shekilngo.
Aidha, Mkuu wa wilaya ya Ubungo Albert Msando amesema serikali inaendelea na kutimiza maerekezo yote ya viongozi ikiwa pamoja na oparesheni za kiusalama katika kituo cha stendi ya magufuli.
Mradi wa stendi ya mabasi ya magufuli ni kituo kilicho jengwa kwa lengo la kupunguza hadha na msongamano wa mbasi katikati ya mji huku shabaha kubwa ikiwa ni kuboresha miundombinu ya usafiri nchini n kuweka miundombinu bora kwa wafanyabiashara katika swkta ya usafiri.
Kusuasua kwa matumizi ya Stendi hiyo kwa baadhi ya kampuni za usafiriahaji kunatajwa kuwa ni chanzo cha kupunguza mzunguko wa biashara kituoni hapo sambamba na kuinyima serikali mapato kupitia tozo na makato mbalimbali.
Hivyo kurejea kwa mabasi katika stendi hiyo kutaenda kuchochea uchumi wa halmashauri ya ubungo pamoja na kufungua fursa mpya kwa wafanyabiashara wadogo pamoja na kukuza pato la taifa na mtu mmoja mmoja katika jamii.









Comments
Post a Comment