Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Wananchi mkoani Tanga wametakiwa kuchangamkia fursa zilipo mkoani humu huku wawekezaji wa ndani na nje ya nchi nao wakikaribishwa kuwekeza katika sekta ya madini.
Wito huo umetolewa na kaimu afisa madini mkoa wa Tanga Mhandisi Laurent Bujashi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kufutia fursa zilizo ongezeka katika mkoa kutokana na upanizi wa bandari uliofanywa na serikali.
Mhandisi Bujashi amesema mpaka sasa fursa zilizopo ni kama biashara,utalii,uvuvi,kilimo,huduma, uchukuzi na mawasiliano,viwanda,nishati,ujenzi,fedha,pamoja na madini ambapo katika madini unaweza kujikita kwenye utafiti,uchimbaji,uchongaji,ama uuzaji wa madini.
Aidha Bujashi ameongeza kuwa hadi sasa mkoani Tanga hakuna wachongaji wa madini badala yake hutegemea Vito vilivyo chongwa kutoka mkoani Arusha au Dar es salaam wakati madini mengi hupatikana Tanga.
Bujashi alimalizia kwa kusema kuwa Kila penye mafanikio hapakosi changamoto na mpaka sasa changamoto kubwa katika sekta hii ya madini ni wananchi kukosa mitaji ya kutosha kuwekeza katika madini kwani kunahitajika mtaji mkubwa pamoja na uelewa mdogo wa Sheria ya madini Kwa jamii.
Katika mkoa wa Tanga wilaya zote Zina madini na madini yanayopatikana ni kama vile Rubi,safaya,zicon,chuma,shaba,grafait,chokaa,mchanga,kokoto pamoja na Tanga stone.







Comments
Post a Comment