Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian amewataka wananchi kujitokeza Kwa wingi kesho Agast 18 katika uzinduzi wamaonesho ya wiki ya kitaifa ya elimu ,ujuzi na ufubunifu yanafanyika katika viwanja vya usagara jijini Tanga ambapo mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa elimu,sayansi na teknolojia Mh. Adolf Mkenda.
Aidha Balozi Batilda amesema lengo kuu la maonesho hayo ni kuonyesha mchango wa elimu ujuzi,sayansi, teknolojia na ubunifu katika kufikia malengo mielekoleo/dira ya elimu 2050.
Akizungumza huhusu maandalizi ya maonesho hayo Balozi Batilda amesema mkoa umejipanga vizuri na wapo tayari kumpokea pro. Adolf Mkenda sambamba na washiriki wengine huku ulinzi na usalama ukiimarishwa zaidi.
Katika maonesho hayo pia washiriki zaidi ya 300 wanatarajia kushiriki wakiwemo wawakilishi kutoka vyuo vikuu,vyuo vya mafunzo na ufundi stadi,taasisi za utafiti na maendeleo pamoja na taasisi zinazohusiana na sayansi na teknolojia.
Mkoa wa Tanga umepokea kisai Cha shilingi bilioni 156 kwaajili ya kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.




Comments
Post a Comment