Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga.
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Leo wamefanikiwa kupanda miti isiopungua 1000 katika shule ya sekondari Ummy Mwalimu iliyopo katika kata ya maweni wilayani na hii ikiwa ni muendelezo wa shughuli za kijamii wanazoshiki katika maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwake.
Wakiwa katika zoezi hilo mgeni rasmi Naibu kamishna shughuli za ufundi - Kodi za ndani Ted Frank silkiluwasha amesema TRA pamoja na shughuli ilizonazo lakini pia imekuwa mstari wa mbele katika kushiriki mambo ya kijamii na hii na inadhihisha ushirikiano mzuri uliopo baina ya Mamlaka ya mapato Tanzania na jamii.
Aidha Silkiluwasha pia amesisitiza utunzaji wa miti hiyo kwani Kwa kuilinda itasaidia kuilinda ozone laya,leya inayozuia mionzi ya jua kufika katika uso wa dunia ambayo ni hatari sana Kwa afya ya wanadamu na viumbe vingine vilivyopo.
Sambamba na hilo amemtaka Meneja wa TRA mkoa wa Tanga kuendelea kutoa elimu ya Kodi kwani elimu hiyo inapaswa kuwa endelevu na ili kuboresha hapo amemtaka kuingiza shule hiyo katika ( tax club) lengo kuu la klabu hiyo likiwa ni uhamsishaji katika kulipa Kodi.
Ukiona ukubwa wa taifa sio wingi wa watu au wingi wa silaha bali ni kuwa na uchumi imara,uchumi imara unajengwa Kwa kuwa na mapato ya serikali na hii huwezesha kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo shule,afya na Barabara, hata amani inayotokana na serikali Kwa kuweka ulinzi ni vitu vinategemea mapato",alisema Silkiluwasha.
Kwa Upande wake Meneja TRA mkoa wa Tanga Castrol John amewataka wafanyabiashara kuacha kutumia njia zisizo sahihi pindi wanapoingiza bidhaa na badala yake kulipa Kodi Kwa usahihi.
Castrol pia ameitaka jamii kuwafichua walewote wanaokwepa Kodi na kutangaza donge nono Kwa atakae weza kutoa taarifa zitakazoweza kuokoa mapato ya serikali yanayopotea.
Nae muhifadhi kutoka huduma za misitu (TFS) Michael Charles amezitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa TRA kwa kuwa miti ni muhimu sana katika kutunza viumbe hai sambamba na kutupatia hewan safi,pamoja na kutuingizia kipato kupitia utalii na biashara na kutupatia matunda piakutasaidia kuwa na jamii yenye afya.
Akimalizia Kwa kutoa shukrani Kwa TRA mkuu wa shule ya sekondari Ummy mwalim Asha Kitundu amesema shule inaeneo linalopata heka 700 miti hii itasaidia kuwapatia kivuli na hata kuzuia mmomonyoko wa udongo, pia amewakaribisha wadau wengine kuja kuwaunga mkono katika kuleta maendeleo kwani shule hiyo bado ni changa.
Shule ya sekondari Ummy mwalim ilianzishwa mwaka 2022 ikiwa na wanafunzi 316,ambao walipunguzwa kutoka shule ya sekondari Maweni wakiwa ni kidato Cha 1,2 na 3, mpaka sasa shule hiyo inajumla ya wanafunzi 916 na walimu 3, mwezi wa 7 mwaka huu wanategemea kupokea wanafunzi 83 wa kidato Cha 5.








Comments
Post a Comment