WAZIRI WA FEDHA AONGOZA MBIO ZA SHUKRANI KWA MLIPAKODI KUELEKEA TUZO YA RAIS KWA MLIPAKODI BORA NA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA TRA
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo tarehe 27 Juni 2026 imefanya Mbio na Matembezi ya Shukrani kwa Mlipakodi katika mikoa yote nchini ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuelekea Utoaji wa Tuzo ya Rais kwa Mlipakodi Bora na Maadhimisho ya Miaka 30 ya TRA yatakayofanyika Julai 1, 2026.
Katika Mkoa wa Dar es Salaam, mbio hizo zimefanyika katika Viwanja vya Gymkhana na kuhudhuriwa na watumishi wa TRA, wadau mbalimbali, wafanyabiashara na walipakodi. Mgeni rasmi alikuwa Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omary, Waziri wa Fedha, ambaye aliongoza mbio hizo na kushiriki matembezi ya shukrani pamoja na mamia ya washiriki.
Mbio na matembezi hayo yamefanyika kwa lengo la kutoa shukrani kwa walipakodi kwa mchango wao mkubwa katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali na maendeleo ya Taifa, sambamba na kuhamasisha ushiriki wa wadau katika Maadhimisho ya Miaka 30 ya TRA na hafla ya Tuzo ya Rais kwa Mlipakodi Bora.













Comments
Post a Comment