Mradi huo unafadhiliwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ukiwa ni sehemu ya uwekezaji mkubwa unaolenga kuimarisha miundombinu ya bandari na sekta ya nishati ili kuongeza ufanisi wa uchumi wa Taifa.
Baada ya kukamilika, matanki hayo 15 yatakuwa na uwezo wa kuhifadhi takribani mita za ujazo 378,000 za mafuta, hatua itakayoongeza uwezo wa nchi kuhifadhi mafuta ya akiba, kupunguza muda wa kusubiri kwa meli bandarini, kupunguza gharama za usafirishaji wa mafuta, kuimarisha usalama wa nishati nchini na kuongeza mapato ya Serikali kupitia huduma za bandari. Mradi huo pia unatarajiwa kuifanya Tanzania kuwa kitovu muhimu cha biashara ya mafuta katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.










Comments
Post a Comment