Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

WAZIRI MAKONDA MGENI RASMI USIKU WA SHEREHE ZA MIAKA 25 YA USHIRIKIANO KATI YA CHINA 🇨🇳 NA URUSI🇷🇺.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amehudhuria akiwa ni Mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 25 ya ushirikiano kati ya Urusi na China ambazo zimepambwa na kuitazama filamu ya pamoja kati ya Urusi na China inayoitwa Red Silk (2025), ambapo Makonda amepongeza ushirikiano huo wa miaka 25 wa Mataifa hayo mawili akisema Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano na China na Urusi katika nyanja mbalimbali ikiwemo habari, utamaduni, sanaa na michezo Filamu hiyo imeoneshwa katika Jumba la Urusi Jijini Dar es salaam leo June 24,2026 ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 25 ya ushirikiano wa urafiki mwema kati ya China na Urusi ambapo imewakutanisha pamoja Waigizaji wa Mataifa yote mawili.  Akiongea wakati wa utazamaji wa filamu hiyo, Makonda ambaye ni Mgeni rasmi, amesema Tanzania inayapongeza Mataifa hayo yote mawili kwa kuonesha umuhimu wa ushirikiano wa miaka 25 ambao unachagiza zaidi maendeleo ambapo amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi hizo katik...

LANDMAX YATAJWA KUWA SULUHISHO LA UTAPELI NA MIGOGORO YA ARDHI

 Wananchi pamoja na madalali wa biashara ya ardhi nchini wamehimizwa kutumia huduma za Landmax Real Estate Company Limited ili kufanya miamala ya ardhi kwa usalama, kuondokana na utapeli na kupunguza migogoro inayotokana na biashara zisizo rasmi za ardhi. Wito huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Mbozi na Mkurugenzi wa Landmax Real Estate Company Limited, Onesmo Mnkondya, wakati wa uzinduzi wa ofisi za kampuni hiyo uliofanyika Juni 24, 2026 jijini Dodoma. Mnkondya amesema Landmax imeanzishwa kwa dhamira ya kuleta mapinduzi katika sekta ya ardhi na mali isiyohamishika kwa kutoa huduma za kitaalamu, zinazozingatia sheria na zinazolenga kulinda maslahi ya wananchi na wawekezaji. Amesema kupitia kampuni hiyo, wananchi watapata huduma za uuzaji na ununuzi wa ardhi na mali isiyohamishika, ushauri wa uwekezaji, usimamizi wa mali, urasimishaji wa nyaraka za ardhi, uendelezaji wa miradi, tafiti za soko pamoja na ushauri wa kitaalamu unaowezesha uwekezaji wenye tija. "Tunawaalika wananchi na...

TANZANIA: HISTORIC IPU TRANSITION PUTS GENDER MILESTONE AT HEART OF 'GENEVA OF AFRICA' ARUSHA ASSEMBLY

 By Prosper Makene GENEVA, — The Inter-Parliamentary Union is entering a historic transition that will reshape the world’s oldest international parliamentary body. Secretary General Martin Chungong will conclude his tenure at the end of June and formally hand over to Ambassador Anda Filip, who becomes the first woman to serve as Secretary General in the IPU’s 130-year history. The handover marks the end of Chungong’s decade-long leadership, during which he championed parliamentary strengthening, youth participation, and gender equality across member parliaments. His successor, Ambassador Anda Filip of Romania, brings extensive multilateral experience to the role. She previously served as Permanent Representative to the UN in Geneva and has been a vocal advocate for institutional reform and inclusive governance. IPU President Dr. Tulia Ackson of Tanzania is expected to chair the Executive Committee session in Geneva that will oversee the transition. Dr. Ackson herself made history i...

MASHINDANO YA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NCHINI KUUNGURUMA JULAI 6-2026

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Michuano ya CDF CUP 2026 amesema michuano hiyo inatarajiwa kuanza rasmi julai 6 huku lengo likiwa ni kuwaonesha watanzania namna jeshi lao linavyokuza na kuibuq vipaji mbalimbali. Akizungumza mapema hii leo, Brigedia Jenerali Saidi Hamis Saidi katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akielezea maandalizi ya michuano hiyo ambapo pia amesema mikakati ya jeshi la Wananchi wa Tanzania ni kuimarisha timu za kijeshi ili kutoa wawakilishi wazuri ndani na nje ya nchi. Aidha, Brigedia Jenerali Saidi amesema kuwa katika michuano ya mwaka huu jeshi limefanikiwa kufanya maboresho kwa kuja na zawadi za mikanda kwa washindi ikiwa pamoja na kuongeza mchezo wa 'Pool Table' ili kuongeza wigo wa washiriki katika mchezo huwo. Katika hatua nyingine, Brigedia Jenerali Saidi amesema kuwa miongoni mwa michezo itakayo shindaniwa ni pamoja na mpira wa miguu, Pool Table, Mchezo wa Mishale, ikiwa pamoja na michezo yote ya mikono. Kwa up...

MTUHUMIWA WIZI WA MTOTO MCHANGA AKAMATWA LUSHOTO

 Na Mwanamkuu Mwandoro,Lushoto. Jeshi la polisi mkoani Tanga limemtia mbaroni mtuhumiwa wizi wa mtoto mchanga katika hospitali ya wilaya ya Lushoto aliyefahamika Kwa jina la Habiba Fundi. Akizungumza na waandshi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Juni 21,2026,saa Moja usiku katika kitongoji Cha Gerekaya,Kijiji Cha kwemashai wilayani Lushoto akiwa na mtoto huyo.  Mchunguzi amesema Juni 19,majira ya saa Moja jioni mama mzazi wa mtoto huyo Mwanaidi Nyaki ,mkazi wa Kijiji Cha Kwemakame aliripoti kupotelewa na mtoto wake wa siku Moja. Kamanda mchunguzi amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa mwanamke huyo ambaye hakufahamika Kwa wakati huo alijenga ukaribu na mama mzazi pamoja na ndugu walikuwa wakimuhudumia hospitalini,na baada ya kujenga urafiki na kuaminiwa alitumia fursa hiyo kumchukuwa mtoto huyo mchanga na kumuweka kwenye beseni lenye nguo na kutoweka nae. Aidha kamanda huyo pia aliongeza kuwa aliidanganya f...

MHANDISI SAMAMBA AWATAKA WATENDAJI WA TUME YA MADINI KUIMARISHA USIMAMIZI WA SEKTA YA MADINI*

Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa watakiwa kuharakisha utatuzi wa migogoro na kusimamia matumizi bora ya leseni za madini_ 📍MOROGORO Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, amewataka watendaji wa Tume ya Madini nchini kuendelea kuimarisha usimamizi wa Sekta ya Madini kupitia usimamizi madhubuti wa leseni za madini, utatuzi wa migogoro kwenye uchimbaji wa madini pamoja na kuongeza ushiriki wa Watanzania katika shughuli za mnyororo wa thamani wa madini ili sekta hiyo iendelee kutoa mchango mkubwa katika Pato la Taifa. Akizungumza katika kikao cha Menejimenti ya Tume ya Madini kilichofanyika mkoani Morogoro, Mhandisi Samamba amesisitiza umuhimu wa Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kuhakikisha leseni zinazotolewa kwa wachimbaji zinaendelezwa kwa mujibu wa masharti ya leseni hizo, akibainisha kuwa Serikali haitasita kufuta leseni zisizoendelezwa na kuzipatia kwa wawekezaji au waombaji wenye uwezo na dhamira ya kuziendeleza. Aidha, amewataka Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kushugh...