WAZIRI MAKONDA MGENI RASMI USIKU WA SHEREHE ZA MIAKA 25 YA USHIRIKIANO KATI YA CHINA 🇨🇳 NA URUSI🇷🇺.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amehudhuria akiwa ni Mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 25 ya ushirikiano kati ya Urusi na China ambazo zimepambwa na kuitazama filamu ya pamoja kati ya Urusi na China inayoitwa Red Silk (2025), ambapo Makonda amepongeza ushirikiano huo wa miaka 25 wa Mataifa hayo mawili akisema Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano na China na Urusi katika nyanja mbalimbali ikiwemo habari, utamaduni, sanaa na michezo
Filamu hiyo imeoneshwa katika Jumba la Urusi Jijini Dar es salaam leo June 24,2026 ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 25 ya ushirikiano wa urafiki mwema kati ya China na Urusi ambapo imewakutanisha pamoja Waigizaji wa Mataifa yote mawili.
Akiongea wakati wa utazamaji wa filamu hiyo, Makonda ambaye ni Mgeni rasmi, amesema Tanzania inayapongeza Mataifa hayo yote mawili kwa kuonesha umuhimu wa ushirikiano wa miaka 25 ambao unachagiza zaidi maendeleo ambapo amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi hizo katika kuhakikisha urafiki ustawi wa raia wa Mataifa yote matatu unazidi kuimarika katika nyanja mbalimbali ikiwemo za sanaa, utamaduni, michezo na habari.
Usiku huu umeandaliwa na ubalozi wa China nchini Tanzania na Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania wakiongozwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian na Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Andrey Avetisyan ambao ndio wenyeji wa usiku huu ambapo wamewaalika Viongozi wa Serikali ya Tanzania wakiongozwa na Waziri Makonda pamoja na Maafisa wa Bodi ya Filamu ikiwa ni sehemu ya kuthamini ushirikiano wa nchi hizo na Tanzania.
























Comments
Post a Comment