Na Mwanamkuu Mwandoro, Tanga
Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa ilikuweza kutimizandoto zao na kukuza vipaji kwani bila kufanya hivyo watabaki kuona maisha magumu Kila siku.
Hayo yamesemwa na mkurungenzi mtendaji wa kituo cha kulea na kukuza vipaji kwa upande wa soka Mohamed Mgandi kilichopo wilayani Korogwe Cha KOROGWE YOUTH SOCCER CENTER ambacho mpaka sasa kina mwaka mmoja.
Mgandi amesema lengo la kituo hicho ni kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vilivyopo kwani mpira sasa ni biashara na ili iweze kuuzika ni lazma ipikwe vizuri kuanzia hatua za awali.
"Vipaji ni vingi sana ,Kwa kuliona hilo tukaona tuanzishe kituo ambacho kitazalisha wanasoka Bora na wenye ujuzi wa kutosha kwani sisis tuna pokea watoto kuanzia umri wa miaka sita mpaka kumi na sita (6-16),hapa utaona mtoto huyo lazima awe Bora kwani tunaanza kumpika angali bado mchanga kabisa", alisema Mgandi.
Aidha kituo hicho pia kimekuwa kikishirikiana na vituo vingine katika kuendeleza vipjia ikiwemo Azam na mpaka sasa wamesha peleka vijana watatu kwenda Azam na vijana saba wapo katika vilabu mbalimbali vya soka vinavyocheza ligi daraja la pili.
Mgandi pia amewataka wazazi na walezi kutowafungia watoto kwani Kwa kufanya hivyo watakuwa hawawatendei haki.
Akizungumza Kwa niaba ya vijana wanaolelewa katika kituo hicho Shafii Waziri amesema kituo hakibagui mtu kutoka sehemu yoyote Ile kwani wapo mpaka vijana kutoka nje ya nchi muhimu ni kuwa na nidhamu na upendo.
"Kituoni hakuna ubaguzi kabisa kwani tupo watu wa kutoka sehemu mbalimbali na tunaishi vizuri tu kinachozinhatiwa hapa ni nidhamu ya mtu kwani hakuna mafanikio kama mtu hauna nidhamu na pia walimu nakuwa wakitufatilia mpaka shuleni ili kuweza kujiridhisha na mienendo yetu", Waziri
Korogwe youth soccer center wanakakaribisha wadau ili kuwashika mkono kwani Kwa asilimia kubwa bado watoto wanajihudumia Kwa kuchangishana.









Comments
Post a Comment