Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo wamefanya mazungumzo na ujumbe maalum wa Wajumbe 11 wa Baraza la Wawakilishi la Marekani (Congress) kutoka Vyama vyote viwili Vikuu nchini Marekani, ulioongozwa na Ronny Jackson, Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya ya Huduma za Kijeshi, Ulinzi na Usalama ya Baraza la Wawakilishi la Marekani (House Armed Services Subcommittee).
Mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi za Makao Mkuu ya zamani ya Jeshi la Wananchi la Tanzania, Ngome Upanga, Dar es Salaam, ymelenga kujadili maeneo ya kipaumbele katika uhusiano kati ya Tanzania na Marekani, hususan ushirikiano wa biashara, uwekezaji, ulinzi na usalama pamoja na hali ya amani na usalama katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Wakati wa mazungumzo hayo Marekani, imeonyesha dhamira ya kupanua ushirikiano katika biashara na uwekezaji, hususan katika sekta za kimkakati zikiwemo gesi asilia (LNG), Madini muhimu, usafiri wa anga, ulinzi na usalama.
Aidha, Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano baina ya wananchi wa nchi hizo mbili kwa kuondoa vikwazo vya visa kwa Watanzania wanaosafiri kwenda Marekani pamoja na Vikwazo vingine ambavyo Marekani iliiwekea Tanzania.
Ujumbe wa Marekani umeipongeza Tanzania kwa mchango wake katika kudumisha amani na usalama wa kikanda, ikiwemo juhudi za kupambana na ugaidi na ushiriki katika operesheni za kulinda amani barani Afrika.








Comments
Post a Comment