Na Mwandishi Wetu, Dodoma Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imetangaza kuanza kwa utekelezaji wa miradi mipya zaidi ya 30 ya umwagiliaji katika mwaka wa fedha 2026/2027, sambamba na mpango wa kugawa zaidi ya pampu 2,000 za umwagiliaji na kuajiri kati ya vijana 2,000 hadi 4,000 kupitia miradi ya uchimbaji wa visima nchini. Hatua hiyo inalenga kuongeza uzalishaji wa mazao, kupunguza utegemezi wa mvua na kuimarisha mchango wa sekta ya kilimo katika ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Malecela jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Raymond Mndolwa, alisema Serikali imejipanga kuhakikisha wakulima wanapata miundombinu ya kisasa ya umwagiliaji ili kuongeza tija katika uzalishaji. "Lengo letu ni kuhakikisha mkulima wa Tanzania anazalisha kwa tija mwaka mzima bila kutegemea mvua. Umwagiliaji ni msingi wa kilimo cha kisasa na chenye tija," alisema Mndolwa. Alis...
Marato tv - Sauti ya Jamii