Na Dawati la Habari Polisi Mwanza Jeshi la Polisi Wilaya ya Nyamagana limewataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani na usalama wa jamii kwa kushirikiana kwa karibu na vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na serikali za mitaa katika kuwabaini na kuwafichua wahalifu wanaojificha kwenye maeneo yao. Wito huo umetolewa Julai 26, 2026 na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nyamagana, SSP Virginia Sodoka, wakati wa fainali za mashindano ya Polisi Jamii Cup zilizofanyika katika Kata ya Mirongo, ambapo Mashi FC ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga Mirongo FC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mirongo. Akizungumza mbele ya mamia ya wananchi na mashabiki wa soka waliojitokeza kushuhudia fainali hizo, SSP Sodoka alisema vijana ni nguvu kazi ya taifa na nguzo muhimu katika kuhakikisha mfumo wa Polisi Jamii unafanikiwa. "Vijana wana nafasi kubwa ya kuwa walinzi wa amani katika jamii. Mkiamua kushirikiana na Jeshi la Polisi mtasaidia kuzuia uhalifu kabla haujatokea. Lakini pia msipo...
Marato tv - Sauti ya Jamii