Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Atembelea na Kukagua Mabanda ya Wadau wa Maendeleo Katika Sekta ya Afya Wanaoshirikiana na Serikali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akitembelea na kukagua mabanda ya wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya wanao shirikiana na Serikali pamoja na Taasisi ya Benjamini Mkapa katika utoaji wa huduma za Afya baada ya kuwasili kwenye Mkutano wa kumbukizi wa Hayati Mkapa unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar Es Salaam.  Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameambatana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Mawaziri wa Serikali ya Tanzania na Zanzibar akiwemo Waziri wa Afya Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui pamoja na mgombea mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Afrika Dkt. Faustine Ndugulile.  Rais Dkt. Samia anatarajia kulifunga Kongamano hilo la kumbukizi la Rais Mstaafu Mhe. Benjamini Mkapa leo Julai 31, 2024 ambalo limewakutanisha wadau wa maendeleo katika Sekta ya Afya kutoka ...

Nafasi za Kuandikishwa Jeshini

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ), Limetangaza Nafasi za kuandikishwaJeshini Kwa Vijana wa kitanzania wenye Elimu ya Kidato Cha nne na Kidato Cha Sita. Aidha uandikishaji utahusisha Vijana waliopo Katika makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa " Operesheni Jenerali Venance Mabeyo"  na waliomaliza Mkataba ambao wameifanya Mafunzo ya JKT Kwa mujibu wa Sheria na Kwa Mkataba wa kujitolea.

Rais Ruto Amteua Dorcas Oduor Kuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya

Iwapo ataidhinishwa na bunge Dorcas Agik Oduor atakuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza mwanamke nchini Kenya Oduor, ambaye kwa sasa anahudumu kama Katibu wa Mashtaka ya Umma katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP), ni wakili wa Mahakama ya Juu mwenye Shahada ya Uzamili ya Kudhibiti Migogoro ya Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na Shahada ya sheria kutoka chuo hicho. Kabla ya uteuzi wake, Oduor alishikilia nyadhifa mbali mbali katika Ofisi ya Mwendesha Mashtaka ya ODPP ikiwa ni pamoja na Naibu Mkurugenzi, Mkuu wa Idara ya uhalifu wa kiuchumi, kimataifa, Naibu mwanasheria mkuu wa serikali, na Wakili wa serikali katika ofisi ya mwanasheria mkuu. "Wakili Mkuu Oduor amedhihirisha uadilifu , umahiri wa kitaalamu na kujitolea kwa uthabiti kwa utawala wa sheria. Iwapo ataidhinishwa na Bunge la taifa, Dorcas Agik Oduor atakuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza mwanamke katika taifa la Kenya," taarifa ya Ruto kwa Baraza la Mawaziri, iliyoandikwa na Mkuu wa Wafanyakazi katika of...

Ziara ya Dkt Nchimbi Mikoa ya Kusini Yavuna Wanachama Wapya Toka ACT, CUF na CHADEMA

  Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, inayoendelea katika mikoa ya Kusini, akianzia Mtwara na sasa yuko Lindi, imewahamisha viongozi waandamizi wa vyama vya ACT Wazalendo, CUF na Chadema walioamua kujiunga CCM leo, wakisindikizwa na mamia ya wanachama waliorejesha kadi zao za vyama vya zamani kwa kasi kubwa kwenye mkutano wa hadhara.  Katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mpilipili, Lindi mjini, ukiwa ni mwendelezo wa ziara ya Balozi Nchimbi, amewapokea viongozi hao waandamizi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Lindi na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mchinga Ndugu Hamidu Bobali. Viongozi wengine ni pamoja Mwenyekiti wa Wanawake wa ACT Wazalendo Lindi Mjini Bi. Hawa Kipara, Meneja Kampeni wa Wabunge ACT Wazalendo Lindi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana CUF Lindi Issa Sapanga, Katibu wa ACT Wazalendo Mkoa wa Pwani, Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Mchinga, Mwenyekiti wa Wanawake Chadema Li...

Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Sengerema Awaasa Vijana Kushiriki Katika Uchaguzi

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya Sengerema Patrick M. Mundeba, amewataka vijana kutokukatishwa tamaa na watu wanaoamini fedha ndiyo kila kitu kwenye uchaguzi, hivyo kuvunja nia ya vijana kutia nia kwenye nafasi mbalimbali za uchaguzi ikiwemo serikali za mitaa mwaka huu 2024. Mundeba ameyasema hayo wakati wa kufunga Kambi ya Mafunzo maalumu ya Vijana wa itifaki na hamasa iliyofanyika Kwa muda wa siku saba "Amesema  wakati wa Mungu hauna maskini wala tajiri, muda ukifika kijana jipime kachukue fomu gombea Mungu atatuma malaika waje kukusaidia utashinda Vijana hatupaswi kuwa na haraka kwasababu kwa umri wetu huu hatuwezi kuchelewa" Amesema Mundeba

MUWASA Yajipanga Kuongeza Huduma ya Upatikanaji wa Maji Safi na Salama Kwa Asilimia 98

Na Shomari Binda- Musoma Mamlaka ya Maji  Safi na Usafi wa Mazingira Musoma( MUWASA) imejipanga Kuongeza Huduma ya upatikanaji wa maji safi na Salama Kwa Wananchi Kupitia Mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji kwenye  mitaa 7 ya pembezoni manispaa ya manispaa ya Musoma unakusudiwa kuhudumia watu 40,000. Mitaa iliyopo kwenye mradi huo na watu wake kupata huduma hiyo ya maji ni Kwangwa A na B, Kiara, Songambele, Nyabisare, Bweri na Bweri Bukoba. Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) Mhandisi Nicas Mugisha, wakati akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Godfrey Mnzava leo julai 30 ulipotembelea mradi huo. Amesema mradi huo unaoghalimu kiasi cha milioni 600,000,000 ulianza novemba 2023 na unatarajiwa kukamilika novemba 2024. Nicas amesema lengo la mradi ni kuongeza upatikanaji wa maji kwa wananchi wa manispaa ya Musoma kutoka asilimia 95 na kufikia 98. " Ndugu kiongozi wa mbio za mwenge mradi huu utakapokamilika utahu...