Mwenyekiti wa UVCCM wilaya Sengerema Patrick M. Mundeba, amewataka vijana kutokukatishwa tamaa na watu wanaoamini fedha ndiyo kila kitu kwenye uchaguzi, hivyo kuvunja nia ya vijana kutia nia kwenye nafasi mbalimbali za uchaguzi ikiwemo serikali za mitaa mwaka huu 2024.
Mundeba ameyasema hayo wakati wa kufunga Kambi ya Mafunzo maalumu ya Vijana wa itifaki na hamasa iliyofanyika Kwa muda wa siku saba
"Amesema wakati wa Mungu hauna maskini wala tajiri, muda ukifika kijana jipime kachukue fomu gombea Mungu atatuma malaika waje kukusaidia utashinda
Vijana hatupaswi kuwa na haraka kwasababu kwa umri wetu huu hatuwezi kuchelewa" Amesema Mundeba

Comments
Post a Comment