Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tanzania Kufanya Mageuzi Makubwa Sekta Ya Ardhi-Ndejembi

SERIKALI ya Tanzania imetangaza mageuzi makubwa ya sekta ya ardhi yanayolenga kuboresha usimamizi, kuchochea ukuaji wa uchumi, na kulinda haki za wananchi wake.  Akizungumza katika siku ya pili Mkutano wa Kimataifa wa Sekta ya Ardhi ulioandaliwa na Benki ya Dunia katika Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Washington DC, Marekani Mei 06, 2025, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi amesema mageuzi hayo yamefanywa na Serikali kupitia Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995 (Toleo la Mwaka 2023) ambayo ilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Machi 17, 2025 jijini Dodoma. Waziri Ndejembi amesema Sera hiyo inalenga kuboresha usimamizi wa ardhi kwa kuweka msingi imara wa haki, usawa na matumizi endelevu ya rasilimali hiyo muhimu.  ‘‘Mageuzi haya yanatokana na uhitaji unaoendana na mahitaji ya sasa ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kukabiliana na changamoto kama migogoro ya ardhi, ukuaji wa mijini na mabadiliko ...

Waziri Mavunde Atangaza Kiama Kwa Kampuni 95 za Uchimbaji Madini

   ▪️Yatoa hati za makosa kwa kukiuka masharti ya Leseni ▪️Kampuni 7 tu kati ya 95 ambazo hazijaanza uchimbaji zimelaza mtaji wa Trilion 15  ▪️Zapewa siku 30 kujibu hoja *Dar Es Salaam* SERIKALI  imetoa Hati za Makosa kwa Kampuni  95 za Uchimbaji Mkubwa na wa Kati wa Madini kutokana na wamiliki wa leseni hizo kukiuka masharti ya Leseni  kama yalivyoainishwa kwenye Sheria ya Madini. Akizungumza leo Mei 6, 2025 jijiini Dar es Salaam, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde amesema kampuni hizo zinapaswa kujibu hoja ndani ya siku 30 la sivyo zitafutiwa leseni zao. Hati hizo za makosa zimetolewa rasmi kuanzia Aprili 14, 2025 na muda wake utamalizika Mei 13 mwaka huu.   “Kama wanahoja walete majibu yao, tuyahakiki tukijiridhisha na hoja zao tutawaondolea makatazo kama hawana hoja tutawafutia leseni zao kwa  mujibu wa Sheria ya Madini Sura 123  ya  utoaji na ufutaji wa leseni za  madini na uchimbaji kifungu cha 63 na Kanuni zake, amba...

Vijana Urafiki Vicoba Musoma Wakumbushwa Kujiwekea Akiba

Na Shomari Binda-Musoma  VIJANA wa group la Urafiki Vicoba waliopo Musoma wamekumbushwa umuhimu wa kujiwekea akiba kupitia hisa na michango mingine. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kikundi hicho Makongoro Abdi alipokuwa akizungumza na wanachama jana mei 4,2025. Amesema kujiwekea akiba ni suala la msingi kutokana na changamoto za maisha na kuwa katika umoja kunasaidia kubadilishana mawazo. Makongoro amesema lengo la kuanzishwa kwa umoja huo ni kusaidiana kwa shida na raha na kuwahimiza wanachama kupendana na kuwa wamoja. Amesema uwekaji wa akiba na ununuaji wa hisa utawezesha kwa baadae kupata mikopo nafuu kupitia umoja huo na kujiinua kiuchumi. " Niwakumbushe vijana wenzangu upo umuhimu mkubwa wa kujiwekea akiba na ununuaji wa hisa ambao tunaendelea nao hivi sasa. " Kwa kuwa ndio tunaanza umoja wetu baadae uwekezaji tunaoufanya utatusaidia kukopeshana kupitia kikoba chetu na kujiinua kiuchumi",amesema. Mweka hazina wa kikundi hicho Joseph Misana amesema fedha za ki...

Mjumbe wa Kamati Kuu Ccm, Leila Ngozi Awasili Bariadi Kusimamia Uwasilishaji Wa Ilani ya Chama – “ccm Inatenda, na inaeleza, "

BARIADI, SIMIYU  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Mlezi wa Mkoa wa Pwani, Leila Ngozi, amewasili rasmi katika Jimbo la Bariadi kwa ziara maalum ya kusimamia na kushuhudia uwasilishaji wa Ilani ya CCM 2020–2025, hatua inayolenga kuimarisha uwajibikaji wa viongozi na kuonesha utekelezaji wa ahadi kwa wananchi. Katika ziara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew, Mbunge wa Jimbo la Bariadi, amepewa jukumu la kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani hiyo mbele ya Mjumbe huyo wa Kamati Kuu, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Bariadi, na viongozi mbalimbali wa chama na serikali. > “Leo Bariadi tunajivunia kupata heshima ya kupokea kiongozi wa juu wa Chama – Mjumbe wa Kamati Kuu. Huu ni uthibitisho kuwa CCM haiteleki maeneo yake – na kila ahadi iliyotolewa kwa wananchi ni agizo linalopimwa kwa vitendo,” alisema mmoja wa wajumbe wa mkutano huo. Tukio hilo limeambatana na mapokezi makubwa na msisimko wa kisiasa, ambapo viongozi wa mashina, kata, tarafa na wilaya w...

Wakigawa Jimbo Nitagombea Bariadi Vijijini-Eng Kundo

BARIADI, Simiyu  Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi Kundo Mathew, ametangaza kuwa endapo Jimbo hilo litagawanywa rasmi, atagombea tena Ubunge kupitia Jimbo la Bariadi Vijijini – eneo analotokea na analosema lina uhitaji mkubwa wa maendeleo ya karibu. Akizungumza leo katika Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Bariadi uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Bariadi Alliance, Mhandisi Kundo aliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020–2025 mbele ya wajumbe wa mkutano huo, huku akitumia jukwaa hilo kueleza dhamira yake ya kuendelea kulitumikia Taifa kupitia mzizi wake wa kijijini. > "Kuna mkakati wa kugawa Jimbo la Bariadi kutokana na ukubwa wake wa kata 31. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imefika kukusanya maoni na sisi kama viongozi tumeonyesha nia njema ya kupendekeza mgawanyo huo ili kurahisisha shughuli za maendeleo na kuwasogezea wananchi huduma muhimu," alisema Mhandisi Kundo. Aidha, alieleza wazi kuwa iwapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania a...

Nmb Yakabidhi Vifaa Vya Milioni.42.4 Kigoma,Wadau Wahimizwa Kuunga Mkono Serikali

OR-  TAMISEMI Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI Mhe. Zainabu Katimba  amepokea Vifaa vyenye thamani ya shilingi Mil.42.4 kwa ajili ya huduma za Afya na Elimu kutoka Benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya benki hiyo kurejesha kwa Jamii. Akipokea vifaa hivyo Mhe. Katimba amesema serikali inaendelea kuhakikisha inapeleka maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya,Elimu na miundombinu hiivyo amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kuwaletea maendeleo wananchi.  “Tuwashukuru sana wadau wetu wakubwa wa NMB tunatambua jitihada zenu za kuunga mkono serikali kwa juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita katika sekta nyingi ikiwemo Afya na Elimu” amesema Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa na Kaimu meneja wa NMB kanda ya Magharibi Gardiel Sawe ni vifaa vya kujifungulia, Viti  vitano (05) kwa ajili ya Wagonjwa, Vitanda kumi (10) kwa ajili ya Wajawazito kujifungulia  ambavyo vyote vimetole...