Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea mradi wa Uwanja wa AFCON Fumba kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wake.
Ziara hiyo ya ukaguzi imefanyika leo, tarehe 14 Juni 2026, ambapo Rais Dkt. Mwinyi ametembelea maeneo mbalimbali ya uwanja huo wa kisasa unaojengwa na Kampuni ya Orkun Group ya Uturuki unaotarajiwa kutumika katika Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2027.
Rais Dkt. Mwinyi ameendelea na utaratibu wake wa kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Nchi tatu za Afrika Mashariki, Tanzania, Kenya na Uganda, zinatarajiwa kuandaa kwa pamoja Michuano ya AFCON 2027. Uwanja wa AFCON Fumba ni miongoni mwa viwanja vinavyotarajiwa kutumika katika michuano hiyo.










Comments
Post a Comment