📌Tarura Yapokea Tuzo Tatu za PPRA
Arusha
TARURA Mkoa wa Lindi imepata tuzo ya Ukidhi wa Sheria ya Ununuzi wa Umma kufuatia ukaguzi wa utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Tuzo hiyo imetolewa katika Kongamano la 10 la Ununuzi wa Umma, ikiwa ni kutambua uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za ununuzi wa umma pamoja na kuimarisha uwazi, uwajibikaji na usimamizi bora wa rasilimali za umma.
TARURA Lindi inaendelea kujidhatiti katika kuhakikisha utekelezaji wa majukumu yake unazingatia misingi ya utawala bora na matumizi yenye tija ya fedha za umma.

Comments
Post a Comment