Na Shomari Binda-GMTV
WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii.
Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii.
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho.
Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii.
" Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti.
" Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni kila wakati januari hadi januari na kwa kuwa tunajua ni kada wa Chama cha Mapinduzi akija kugombea tutamchagua",amesema.
Kwa upande wake Warioba Samwelly mkazi wa Mugumu amesema Dkt.Nyansaho amewezesha kusukuma usambazaji wa umeme vijijini Serengeti kama wilaya ni ya kwanza katika kanda ya ziwa kwa usambazaji wa umeme vijijini kupitia mahusiano yake na Tanesco na kuwa jambo la mfano.
Kupitia mahusiano hayo mema kwa upande wa wawekezaji ndani ya Hifadhi na shirika la TANAPA, amewashawishi na kupitia ujirani mwema shirika limejenga mabweni ya wanafunzi shule za sekondari kiu yake kubwa ikiwa kupandisha ufaulu na taaluma bora.
" Nyansaho Foundation imewezesha kukabidhi "ULTRA SOUND"katika kituo kongwe cha afya tangu uhuru cha Iramba Tarafa ya Ngoreme kilichokuwa kikihudumia wakazi zaidi ya tarafa ya Ngoreme na Ikorongo changamoto kubwa ilikuwa ukosefu wa kifaa-tiba hicho muhimu katika uchunguzi wa afya ya mama na mtoto hasa kipindi cha ujauzito.
" Ameweza kuokoa maisha ya watoto wachanga na kuokoa maisha ya Mama wajawazito kwa kupatikana kwa kifaa hiki imekuwa ukombozi tunamuombea Mungu",amesema.


.jpg)



Comments
Post a Comment