Waziri Mkuu Akagua Ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga

GEORGE MARATO TV
0


WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Machi 08, 2026 amekagua maendeleo ya ukarabati na uboreshaji wa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga uliopo mkoani Rukwa.

Mradi huo ulianza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 kwa gharama ya shilingi bilioni 60.1 na hadi sasa umefikia asilimia 96 ya utekelezaji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Dkt. Mwigulu amewapongeza wananchi wa Rukwa kwa kupata uwanja wa ndege wa kisasa kwa kuwa maendeleo hayo yanaonesha mabadiliko makubwa ya mkoa huo.









Amesema kuwa kwasasa Rukwa siyo ile ya zamani bali ni Rukwa ya kisasa na ya viwango, inayokwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya taifa.

Aidha, amesema miradi ya aina hiyo ndiyo mafanikio ambayo Serikali ya Awamu ya Sita inajivunia kwa kuwekeza katika miradi ya maendeleo yenye tija na inayoacha alama kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Ukarabati na upanuzi wa uwanja huo unatarajiwa kuimarisha huduma za usafiri wa anga katika Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini pamoja na kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii.

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameanza ziara ya kikazi katika mkoa wa Rukwa ambapo atakagua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top