Waziri Mkuu Akagua Ujenzi wa Soko la Kisasa la Mazao Kanondo-Rukwa

GEORGE MARATO TV
0


WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Machi 8, 2026 ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Kisasa la Mazao Kanondo lililopo Sumbawanga mkoani Rukwa.

Ujenzi wa soko hilo unatekelezwa kupitia Mradi wa TACTIC kwa gharama ya shilingi bilioni 7.3, na hadi sasa umefikia asilimia 82 ya utekelezaji.


Soko hilo linatarajiwa kuwa kitovu muhimu cha biashara ya mazao, likiwaunganisha wakulima, wanunuzi wakubwa, wasafirishaji na wawekezaji, hatua itakayopanua mtandao wa biashara na kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wa Rukwa na maeneo jirani.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top