Dkt Samia Awapa Furaha Wananchi wa Mkoa wa Mara

GEORGE MARATO TV
0

 


Mgombea kiti Cha Urais Tanzania Kwa tiketi ya CCM na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Katika muendelezo wa ZIARA zake za KAMPENI Mkoa Kwa mkoa,wilaya Kwa wilaya akiwa njiani kuelekea Mkoa wa Mara,wilaya ya Musoma, amesimama kuwasalimu na kuzungumza na wananchi wa Lamadi na Bunda. Awashukuru sana kwa kujitokeza kwa wingi njiani, kwa upendo, dua, sala na baraka.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye kampeni alipokuwa musoma,amegusia afya, elimu, Miundombinu na kilimo,Afya, Mgombea kiti Cha Urais Kwa tiketi ya CCM,Ndg SAMIA SULUHU HASSAN amesema kuwa Serikali itaimarisha uagizaji wa vifaa tiba kikamilifu Katika hispitali zetu,pia upo utaratibu ambao utaratibu wa Ili Kila mwananchi atumie bima ya afya hii itarahisisha upatikanaji Wa tiba Kwa  mwananchi wetu.

Dk.Samia ameendelea kusema kuwa kwenye elimu,Serikali imejitahidi sana kuzingatia elimu bila ada kuanzia darasa la kwanza Hadi kidato Cha Tano na sita,pia Serikali Bado inaendelea maeneo ya kuboresha kwenye elimu.

Mgombea wetu kiti Cha Urais wa Chama Cha Mapinduzi dk. Samia Suluhu Hassan kwenye Miundombinu amesema kuwa anaendelea kusimamia kikamilifu utanuzi wa uwanja wa ndege wa kisasa mjini musoma Mkoani Mara Ili utumike hata Kwa ndege kubwa.







Samia amesema pia kuwa itajengwa reli ya SGR itakayotoka Tanga,Moshi,Arusha hatimaye Kufika Musoma sambamba na reli lakini pia Bandari ya zamani ya Musoma itafufuliwa Ili kupokea meli kubwa itayofanya safari zake kutoka Mwanza,Musoma Hadi Uganda.

Katika sekta za UZALISHAJI amegusia kilimo Cha umwagiliaji na scheme zake kuimarishwa,kuendelea Kutoa mbolea za ruzuku,chanjo,ufugaji,kujengwa mabwawa ya kisasa na kupanua uvuvi wa vizimba Kwa wananchi wa Mkoa wa Mara Kwa kuwa wanapakana na ziwa karibia eneo kubwa.

Rais Samia Suluhu ameshauri wananchi na kuwasihi kuwa ifikapo Tarehe 29.10.2025 Kila mwananchi aende atiki Kwa mama SAMIA bila kuchelewa Ili siku hiyo ushindi upatikane mapema kabisa.

Baada ya maneno hayo ya mgombea Urais aligawa vitabu vya ilani Kwa wagombea ubunge wote wa Jimbo la musoma mjini,musoma vijijini,Tarime mjini,Tarime vijijini na Rorya kisha aliwomba kura Kwa kiti Cha Urais, wabunge na  madiwani,baada ya yote hayo alihitimisha mnamo saa 5.42 jioni kwenye viwanja vya Uwanja wa Karume Musoma Mjini.
















































Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top