Miradi Saba ya Maendeleo yenye Thamani ya Billioni 2.5 kupitiwa na Mwenge wa Uhuru

GEORGE MARATO TV
0

Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 kukimbizwa umbali wa Kilomita 80.3 katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe, Johari Samizi wakati akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mhe, Ngwilabuzu Ludigija mapema Leo tarehe 29/8/2025.

Mhe.Samizi ameeleza kwamba Mwenge wa Uhuru utakagua, Utazindua na kuweka Jiwe la msingi katika Miradi 7 ya Sekta mbalimbali zikiwemo Afya,Elimu, Miundombinu, Nishati, Mazingira, Maji na Vijana yenye gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 2.5.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Ndugu Ismail Ali  Ussi ameridhishwa na utayari na Mapokezi  ya Wananchi wa Wilaya ya Misungwi pamoja na juhudi zinazofanywa na Watendaji katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali na kuwahimiza Wananchi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu Mwezi oktoba mwaka huu na kutimiza haki ya kikatiba ya kupiga kura kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge na Madiwani.

Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge mwaka 2025 "Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu".



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top