-Ni mafunzo ya watendaji wa ccm ngazi za kata na matawi,mbali na mbunge mwenyekiti pia atuhumiwa
Na Shomari Binda;Mara.
MAFUNZO ya watendaji wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Rorya yamedaiwa kuingiliwa na kuvurugwa na viongozi wa chama hicho akiwemo na mbunge.
Viongozi wanaodaiwa kuvuga mafunzo hayo ni mbunge wa jimbo la Rorya Jafari Wambura Chege na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya Ongujo Wakibara wakidaiwa kuiingilia semina ya makatibu wa matawi na kata leo 20/02/2025 na kugawa posho shilingi 50,000 kwa kila katibu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa mitandaoni ukiwa ni pamoja na group la Whassap la CCM mkoa wa Mara zimedai utaratibu huo unakiuka maelekezo kutoka makao makuu ya chama
Taarifa hiyo inadai kuwa mafunzo hayo ya watendaji yasiingiliwe na viongozi au wanasiasa kwa sababu ni mafunzo ya kiutendaji na chama kilisema kitagharamia kila kitu ikiwemo chakula na posho.
"Lengo la chama kufanya hivyo ilikuwa ni kuondoa urasimu wa wagombea kutumia nafasi hiyo kutoa rushwa kinyume chake mwenyekiti wa chama na mgombea wake ambaye ndie mbunge kwa sasa wamevamia ukumbi na kutoa posho hizo.
"Jambo hili halijawafurahisha hata wakufunzi haswa kauli za Mwenyekiti na mbunge baada ya kuzuiwa na wakalazimisha kufanya kwa nguvu",imesema sehemu ya taarifa.
George Marato tv imefatilia taarifa hiyo na kuzungumza na mbunge wa jimbo la Rorya Jafar Chege kwa njia ya simu na kudai yupo msibani toka asubuhi na hajaudhuria kikao hicho na kushangazwa na taarifa hiyo.
Chege amekiri kuiona taarifa hiyo kwenye mitandao na magroup ya CCM lakini hajui lengo lake.
" Nimeshangazwa na taarifa hiyo mimi nipo msibani na nimeambiwa kikao hicho kimeenda vizuri na kimalizika salama hizo taarifa ni za uongo",amesema Chege.
Alipotafutwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya Ongujo Wakibara hakuweza kupatikana kwenye simu na jitihada za kumtafuta kuzungumzia jambo hili zinaendelea.
Baadhi ya wana CCM wamekuwa wakilaani vikali vitendo vya mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rorya kuapa kuwa jina la Chege ndio pekee atakalotembea nalo wakati wa uchaguzi ukifika ndani ya chama.
Kauli hiyo imekuwa ikikalamikiwa na baadhi ya wana ccm na kusema kitendo cha mwenyekiti kuwa na mgombea wake kinaweza kusabisha chuki baada ya kura za maoni na kusababisha chama hicho kupoteza jimbo hilo.
"Mwenyekiti ni wa wote ndio lazima kwa sasa kuwa karibu na mbunge lakini amekuwa akisema kipenga kikipulizwa yeye atakufa na Chege,sasa kauli hizi zinatupa wakati mgumu huko mbele kwa maana ya wana ccm wengine kutotendewa haki"alisema Jarome Otieno
Juhudi za kumtafuta mwenyekiti huyo kuthibitisha madai hayo hazikufanikiwa baada ya simu yake kutopatikana tunaendelea na jitihada za kumtafuta.



Comments
Post a Comment