Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya Uteuzi wa Makamishna wa Jeshi la Polisi.
Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt.Moses Kusiluka,Makamishna Walioteuliwa ni Naibu Kamishna wa Polisi DCP.Kombo Khamis Kombo ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na Kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar,Kuchukua nafasi ya CP.Hamad Khamis Hamad ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.
Naibu Kamishna wa Polisi DCP.Tatu Rashid Jumbe amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na Kuteuliwa kuwa Kamishna wa Utawala na Menejiment ya Rasilimali Watu Katika Jeshi la Polisi,anachukua nafasi ya CP Suzan Kaganda ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.



Comments
Post a Comment