Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Charles Wilson Mahera (Katikati) akiwa na Mwakilishi wa Serikali ya Marekani kutoka idara ya kilimo USDA na Wawakilishi wa shirika lisilo la kiserikali Global Community la nchini Tanzania katika mkutano wa kimataifa unaojadili umuhimu wa kutoa chakula mashuleni.
Mkutano huo ni muhimu sana kwa Tanzania ambapo Tanzania imeanza kutekeleza mradi mpya kutoa chakula mashuleni awamu ya pili Mkoani Mara na Dodoma.
Awamu ya kwanza ilikuwa ni Mkoa wa Mara katika halmashauri za Musoma vijijini, Butiama, Bunda Mjini na halmashauri ya Wilaya Bunda.

Comments
Post a Comment